Pata taarifa kuu

Kenya: Wahuni wenye silaha wavamia shamba la Uhuru Kenyatta

NAIROBI – Watu waliokuwa wamejihami walivamia shamba la rais wa zamani Uhuru Kenyatta na kampuni ya kutengeza mitungi ya gesi, iliyomilikiwa na kiongozi wa upinzani, Raia Odinga.

Uhuru Kenyatta, rais wa zamani wa Kenya
Uhuru Kenyatta, rais wa zamani wa Kenya AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya watu, waliokuwa wamejihami kwa mapanga, walivamia shamba la Kenyatta, Kaskazini Mashariki mwa jiji la Nairobi, wakakata miti na kuiba mifugo kama kondoo.

Wakati wa tukio hilo, maafisa wa polisi hawakuonekana katika êneo hilo la tukio, na saa chache baadaye, miti katika shamba hilo, iliteketezwa moto.

Katika êneo la viwandani jijini Nairobi, vijana waliojihami kwa mawe, walivalmia kampuni ya East Africa Spectrum, inayohusihwa na família ya Odinga na kuishambulia kwa mawe.

Matukio haya mawili, yamekuja siku chache baada ya kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichungwa kunukuliwa akionya kuwa, mali za viongozi hao zinaweza kushambuliwa pia.

Baadhi ya wanasiasa kwenye chama tawala, wamedai kuwa Kenyatta ndiye anayefadhili maandamano ya upinzani dhidi ya Ruto. Kiongozi huyo wa zamani, hajajitokeza kuzungumzia tukio hilo.

Katika hatua nyingine, makundi mawili pinzani katika mtaa wa mabadnda wa Kibera, walikabiliana huku kukiwa na ripoti ya kuteketzwa moto kwa msikiti na Kanisa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.