Pata taarifa kuu

Kenya: Polisi wakabiliana na waandamanaji wa upinzani jijini Nairobi

NAIROBI – Nchini Kenya, Jumatatu ya wiki hii polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha, kuwasambaratisha waandamanaji wa upinzani jijini Nairobi, wakilalamikia kupanda kwa gharama ya maisha na matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka uliopita.Β Β Mwandamanaji mmoja aliuawa baada ya kupigwa risasi na polisi mjini Kisumu, Magharibi mwa nchi hiyo.Β 


Polisi wamekabiliana na waandamanaji wa upinzani jijini Nairobi nchini Kenya
Polisi wamekabiliana na waandamanaji wa upinzani jijini Nairobi nchini Kenya REUTERS - JOHN MUCHUCHA
Matangazo ya kibiashara

Moshi mweupe ulitanda katika mtaa wa Kawangare, polisi wakiurushia msafara wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga, mabomu ya kutoa machozi, kudhibiti maandamano hayo yaliyopigwa marufuku, lakini Odinga alipata fursa ya kuwahotubia wafuasi wake.

β€œGharama ya maisha inapaswa kurudi chini ikiwemo bei ya mafuta na unga. ”amesisitiza Odinga.

00:10

Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya

Hata hivyo, wafuasi wa Odinga hawakufanikiwa kuingia katikati ya jiji la Nairobi, kama ilivyokuwa Jumatatu iliyopita.Waliisia tu kukabiliana na polisi katika mitaa yao na kuteketeza moto matair, kama Elvis Otepa.

β€œBwana Ruto alituahidi elimu bila malipo. Kwa sasa nashindwa kulipa ada ambayo ni zaidi ya Dola 200. Gharama ya usafiri imepanda…Maisha yamekuwa magumu ndio kwa sababu tunaandamana…Tunapigania haki zetu na za watoto wetu. β€œamesema Elvis Otepa

00:16

Elvis Otepa, raia wa Kenya

Reheme Magheni, anahofia iwapo maandamano haya yataendelea kila wiki, uchumi utayumba.

β€œSio Raila au Ruto ndio watakaotupa mahindi, watu wanapaswa kukaa chini na kufanya kazi, na kuachana na haya yanayoendelea.” amesemaΒ Reheme Magheni

00:11

Reheme Magheni, raia wa Kenya

Maeneo mengi ya biashra yalifungwa jana, huku huduma ya treni kutoka katkati mwa jiji kuelekea mitaani ikisitishwa.

Wanahabari kadhaa walijeruhiwa baada ya kushambuliwa na watu waliokuwa wamejihami, kitendo kilicholaaniwa na Baraza la Vyombo Habari nchini humo kama tishio kwa vyombi vaya Habari.

Maandamano ya jana yalifanyia, wakati rais William Ruto akiwa ziarani jijini Berlin nchini Ujerumani, alikokutana na wawekezaji wa nchi hiyo.Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.