Pata taarifa kuu

Kenya: Polisi wa kuzuia ghasia wakabiliana na wafuasi wa Odinga

NAIROBI – Askari wa kupambana ghasia nchini Kenya wamejitokeza kwa idadi kubwa  katika mitaa ya jijini Nairobi na mitaa mingine kama vile Kibera, Mathare na maeneo mengine  katika jitihada za kuzuia maandamano yaliyoitishwa na kipongozi wa upinzani Raila Odinga kupinga kupanda kwa  gharama ya juu ya maisha na masula mengine likiwemo swala la uchaguzi wa mwaka uliopita.

Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya
Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Miji mingine kama vile Kisumu imeshuhudia idadi kubwa ya maofisa wa usalama wanaokabiliana na wafuasi wa Odinga walioiitikia wito wa kinara wao wa kuaandamana kila Jumatatu na alhamis ya kila wiki.

Hadi tukichapisha taarifa hii, Raila Odinga na wanasiasa wengine wanomuunga mkono hawakuwa wanajulikana waliko japokuwa mwishoni mwa juma lililopita, Odinga alisikikza akisema kuwa atakuwa miongoni mwa waandamanji jijini Nairobi.

Maandamano ya leo Jumatatu yanafanyika licha ya inspekta generali wa polisi nchini Kenya, Japeth Koome kueleza kwamba maofisa wake hawataruhusu yafanyike.

Kwa mujibu wa wanahabari wetu kutoka katikati mwa jiji la Nairobi, maduka mengi yamefungwa wamiliki wa biashara haswa maduka ya jumla wakihofia mali yao kuporwa.

Polisi wamesema watawapiga picha waandamanaji na kuwafungulia mashtaka kwa kushiriki maandamano haramu.

Wiki iliyopita, maandamano jijini Nairobi na miji mingine yaligeuka kuwa ghasia, na mtu mmoja aliuawa jijini Kisumu.

Polisi waliwakamata zaidi ya watu 200, wakiwemo wabunge wa chama cha Odinga cha Muungano wa Kenya kutoka mabunge yote mawili.

Wakati wa maandamano ya wiki jana, polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha, ikiwa ni pamoja na msafara wa Odinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.