Pata taarifa kuu

Kenya:Muswada wa marekebisho ya sheria kuhusu maandamano waibua mjadala

NAIROBI – Taarifa ya nia ya wizara ya mambo ya ndani nchini Kenya, kutaka kupeleka bungeni muswada wa marekebisho ya sheria kuhusu ufanyaji maandamano, imeibua mjadala huku ikionekana kuwagawa raia.

Polisi wakukabiliana na ghasia wakiwa katika mtaa kibara jijini Nairobi kukabiliana na wafuasi wa upinzani
Polisi wakukabiliana na ghasia wakiwa katika mtaa kibara jijini Nairobi kukabiliana na wafuasi wa upinzani REUTERS - JOHN MUCHUCHA
Matangazo ya kibiashara

Baada ya maandamano ya juma lililopita ambayo serikali inasema yalikuwa yavurugu, waziri wa mambo ya ndani sasa anataka maboresho ya sheria itakayodhibiti maandamano ya siku za usoni.

Bryan Mutie, ni wakili na mchambuzi wa masuala ya siasa akiwa nchini Kenya amehojiwa na mwandishi wetu Minzilet Ijai kuhusu hatua hii

“Hapa Kenya bado sheria hizo zipo isipokuwa nadhani labda waziri anataka tu kuzitia nguvu.”ameeleza Bryan Mutie.

Wapinzani nchini Kenya wanaona kwamba mapendekezo haya ni njia moja ya serikali kutaka kuminya uhuru wa kufanya mikutano ya kisiasa pamoja na kufanya maandamano ya amani kama inavyokubaliwa katika katiba.

Serikali imekuwa ikiutuhumu upinzani kwa kuendeleza maandamano yanayolenga kuharibu uchumu haswa wakati huu wafanyibiashara wengi wakionekana kufunga biashara zao wakihofiwa kuporwa na waandamanaji.

Aidha Bryan Mutie anaeleza kuwa baadhi ya mapendekezo haya ya waziri wa usalama wa ndani yanalenga kuwakandamiza wapinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.