Pata taarifa kuu

Kenya: Maandamano ya upinzani kuendelea licha ya onyo la polisi:Odinga

NAIROBI – Nchini Kenya, muungano wa upinzani wa Azimio la Umoja, umeitisha maandamano mapya leo jijini Nairobi kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha na kudai kile wanachosema ni ushindi wao wa kisiasa baada ya uchaguzi wa maka uliopita. 

Mrengo wa kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga umepanga kuendelea na maandamano kote nchini kupinga kile kinachotajwa kuwa ni kupanda kwa gharama ya maisha
Mrengo wa kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga umepanga kuendelea na maandamano kote nchini kupinga kile kinachotajwa kuwa ni kupanda kwa gharama ya maisha REUTERS - THOMAS MUKOYA
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, jeshi la Polisi, limeharamisha maandamano hayo. Japhet Koome ni Inspekta Jenerali wa polisi nchini humo. 

“Mimi kama inspekta generali wa polisi hakuna maandamano nimeruhusu, hayo ni mambo ya kisiasa na yanafaa kusuluhishwa kisiasa.” amesisitiza Japeth Koome.

00:24

Japeth Koome, Inspekta Jenerali wa polisi nchini Kenya

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, amewaambia wafuasi wake wajitokeze kwa wingi na kusisitiza kuwa maandamano hayo ni ya amani, akiwa na ujumbe huu kwa polisi.

“Hayo maandamano tunafanya ni ya amani na sheria inakubali”amesema Raila Odinga.

00:25

Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya kuhusu Maandamano

Maandamano ya Jumatatu iliyopita, yalisambaratisha shughuli za kiuchumi jijini Nairobi, na kusababisha pia kifo cha Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Maseno, Magharibi mwa nchi hiyo. 

Wito umekuwa ukitolewa kwa viongozi hao wawili, Rais Ruto na Odinga kuketi pamoja na kutafuta suluhu kama njia moja ya kuliepusha taifa hilo kutumbukia katika mzozo wa kisiasa.

Licha ya wito huo kutoka kwa mashirika ya kiraia na viongozi wa kidini katika taifa hilo la Afrika mashariki, Odinga na Ruto wameonekana kupuuza wito huo na kuendelea na msimamo yao mikali ya kisaisa.

Maandamano ya wiki yanafanyika wakati huu rais William Ruto akiwa nje ya nchi kwa ziara ya siku nne katika mataifa ya Ujerumani na Ubelgiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.