Pata taarifa kuu

Kenya: Watu 238 wakamatwa kufuatia maandamano ya Jumatatu

NAIROBI – Polisi nchini Kenya wamesema watu 238 walikamatwa jana kwenye maandamano ya jana yaliyoongozwa na mrengo wa upinzani wa Azimio la Umoja,kupinga gharama ya juu ya maisha.

Raila Odinga, kinara wa upinzani nchini Kenya
Raila Odinga, kinara wa upinzani nchini Kenya REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Inspekta jenerali wa polisi Japheth Koome, akizungumza siku moja baada ya maandamano hayo,amethibitsha kuwauwa kwa mwanafunzi mmoja wa chuo  kikuu cha Maseno aliyewauwa jijini Kisumu  na kujeruhiwa kwa polisi 31.

Jijini Nairobi, magari kumi ya polisi yaliharibiwa huku maofisa 24 wakipata majereha mabaya.

Kati ya waliokamatwa, 25 walikamatwa katika eneo  la Nyanza, magharibi mwa Kenya ambako maofisa saba walijeruhiwa.

Viongozi sita wa mrengo wa azimio wakiwemo mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi ni miongoni mwa waliokamatwa na baadaye kuachiwa baada ya polisi kushtumiwa vikali kwa kuwakamata waandamanaji na kuwazuia kinyume cha sheria.

Kwa upande wake kiongozi wa Upinzani Raila Odinga, akizungumza, ambapo amelaani polisi kwa kukiuka haki za raia kudai haki zao,ametangaza maandamano hayo yatafanyika siku ya Jumatatu na alhamisi kila wiki ,huku akiwataka wafuasi wake pia kususia huduma za benki ya Kenya Commercial Bank,kampuni ya mawasiliano ya Safaricom ,kampuni ya Radio Afrika inayomiliki pia gazeti la The Star .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.