Pata taarifa kuu

Kenya: Upinzani kufanya maandamano kila siku ya Jumatatu

NAIROBI – Kinara wa muungano wa upinzani nchini Kenya, AZIMIO, Raila Odinga, Jumatatu ya wiki hii alisema watakuwa wanafanya maandamano kila siku ya Jumatatu hadi pale Serikali itakapotekeleza madai yake ikiwemo kushusha gharama ya maisha kwa wananchi.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ameitisha maandamano ya kila siku ya Jumatatu kupinga kupanda kwa gahrama ya maisha.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ameitisha maandamano ya kila siku ya Jumatatu kupinga kupanda kwa gahrama ya maisha. REUTERS - THOMAS MUKOYA
Matangazo ya kibiashara

Odinga alisema haya baada yay eye na wafuasi wake kukabiliana na polisi katika maeneo kadhaa ya jiji kuu, Nairobi.

“Kila siku ya Jumatatu ya kila wiki tutakuwa katika maandamano.”ameeleza Raila Odinga.

00:19

Raila Odinga kuhusu maandamano ya kila Jumatatu

Katika hatua nyingine, rais William Ruto, alimuonya Odinga na wafuasi wao kutotumia vibaya haki za kikatiba walizopewa, akikosoa vurugu za hapo jana.

“Ntahakikisha kama rais kuwa nchi hii inaongozwa na sheria na hakuna kitakachofanyika zaidi ya sheeria, zaidi ya katiba na chochote kile nje ya sheria.”amesisitiza William Ruto.

00:21

Rais wa Kenya William Ruto kuhusu maandamano

Licha ya kuwa sio miji yote ya Kenya ilishuhudia maandamano, ile michache iliyoshiriki, Serikali ilihesabu hasara, ambapo inakadiriwa kiasi cha shilingi za Kenya bilioni 2 kilipotea.

Katika hatua nyengine Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu katika Chuo Kikuu cha Maseno nchini Kenya ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya kitaifa katika  kaunti ya Kisumu.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi marehemu alikuwa miongoni mwa kundi la wanafunzi waliojiunga na waandamanaji wengine ambayo baadaye yaligeuka kuwa ya vurugu.

Wito umeendelewa kutolewa kwa Ruto na Odinga kufanya mazungumzo kama njia moja ya kulinusuru taifa kutumbukia katika ghasia haswa wakati hali ya uchumi ikionekana kuwa mbaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.