Pata taarifa kuu

Kenya: Polisi wakabiliana na waandamanaji wanaopinga mfumuko wa bei za bidhaa

NAIROBI – Polisi nchini Kenya, wametumia mabomu ya kutoa machozi kupambana na waandamanaji wa upinzani, waliojitokeza katikati mwa jijini la Nairobi kukulalamikia kupanda kwa bei ya maisha na kudai kuwa ushindi wake uliibiwa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka uliopita. 

Moafisa wa polisi wamekabiliana na waandamanaji jijini Nairobi
Moafisa wa polisi wamekabiliana na waandamanaji jijini Nairobi AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa polisi waliharamisha maandamano hayo na kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida, lakini mambo yalikuwa tofauti, baada ya wananchi wengi kutojitokeza katikatika ya jiji kuu kwa kuhofia usalama wao. 

Msafara wa kiongozi wa muungano wa upinzani Azimio la Umoja Raila Odinga, ulishambuliwa na vitoa machozi kabla ya kuelekea katika mitaa ya Mashariki mwa jiji la Nairobi kukutana na wafuasi wake. 

Odinga amemshtumu Ruto kwa kutumia maafisa wa usalama kusambaratisha maandamano ya amani aliyosema yataendelea kila Jumatatu. 

“Kazi bado, ndio tumeanza, kila Jumatatu, tutaandamana,” amewaambia wafuasi wake katika mtaa wa Eastleigh nje kidogo na jiji la Nairobi .

Waandamanaji zaidi ya 20 wakiwemo wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na kiongozi wa wachache katika seneti Stewart Madzayo na wabunge wawili wamekamatwa. 

Katika eneo la  Kibera, nje kidogo na jiji la Nairobi, ngome ya wafuasi wa Odinga, watu pia walichoma magurudumu ya magari  huku polisi wakitumia maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji.  

Waandamanaji na polisi pia walikabiliana katika mji wa Kisumu magharibi mwa Kenya, ngome nyingine ya Odinga.  

Katika hatua nyingine, naibu rais Rigathi Gachagua, akizungumza akiwa jijini Mombasa, amemwomba Odinga kusitisha maandamano ambayo amesema, yamesababisha nchi kupata hasara. 

Jijini la Nairobi, limepoteza zaidi ya Shilingi Bilioni 2, tunaomba wapinzania wasitishe maandamano yanayoendelea,” amesema. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.