Pata taarifa kuu

Uganda yajiandaa kuidhinisha sheria mpya dhidi ya wapenzi wa jinsi moja

Uganda itajadili muswada mpya wa kupinga ushoga siku ya Jumatano, amesema Spika wa Bunge, huku nadharia za njama kuhusu suala hilo zikienea kwenye mitandao ya kijamii.

Wanaharakati wa haki za mashoga wanaleta malalamiko dhidi ya sheria mpya, mjini Kampala mnamo Machi 11, 2014.
Wanaharakati wa haki za mashoga wanaleta malalamiko dhidi ya sheria mpya, mjini Kampala mnamo Machi 11, 2014. REUTERS/Edward Echwalu
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na rekodi ya sauti ambayo shirika la habari la AFP liliweza kupata, Annet Anita Among amesema siku ya Jumanne wakati wa mkutano wa kidini: "Kesho tutabeba sheria ya kupinga ushoga."

Bi. Among pia alichapisha video ya mkutano huu kwenye Twitter, akiiongeza kama maoni. "Lazima tulinde kwa wivu maadili yetu na utamaduni wetu." Mahusiano ya watu wa jinsia moja ni kinyume cha sheria nchini Uganda - urithi wa sheria za kikoloni lakini tangu uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1962 hakuna hukumu yoyote iliyotolewa kwa vitendo vya ulawiti vilivyokubaliwa.

Nchi za Magharibi na mashirika ya misaada yanayofanya kazi nchini Uganda yanashutumiwa mara kwa mara kwa “kukuza ushoga” nchini Uganda na mara kwa mara wameitetea jumuiya ya LGBTQ kutokana na mashambulizi yanayohusiana na utambulisho wao katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Katika wiki za hivi karibuni, nadharia za njama zimeongezeka kwenye mitandao ya kijamii, zikihusisha visa vya unyanyasaji wa kingono kwa watoto katika shule za bweni na ushoga kati ya watu wazima. Mwezi uliopita, serikali ilianzisha uchunguzi kuhusu madai ya "kukuza" haki za mashoga, wasagaji na waliobadili jinsia shuleni.

Mnamo 2014, mahakama ya Uganda ilizuia mswada ulioidhinishwa na wabunge na kutiwa saini na Rais Yoweri Museveni ambao ulitaka kuadhibu mahusiano ya jinsia moja na kifungo cha maisha jela. Muswada huo ulizua ghadhabu duniani, huku baadhi ya mataifa wafadhili yakikata misaada kwa nchi hii kufuatia kupitishwa kwa bunge..

Katika rekodi hiyo iliyosikilizwa na AFP, Bi. Among alisema: "Tunawashukuru wahamasishaji wetu wa ushoga kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi waliyoiletea nchi lakini hatushukuru kwa maadili wanayoua."

"Hatuhitaji pesa zao, tunahitaji utamaduni wetu." Frank Mugisha, mkuŕugenzi mtendaji wa Sexual Minorities Uganda, shiŕika kuu la utetezi wa wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda, lililopigwa marufuku tangu mwaka jana, amesema amepokea simu nyingi kutoka kwa watu wa LGBTQ kuhusu sheria iliyopendekezwa. "Wanajamii wanaishi kwa hofu," amesema.

“Vitendo vya ushoga tayari ni haramu na sheria mpya itamaanisha unyanyasaji na ubaguzi zaidi dhidi ya watu ambao tayari wako hatarini.”

Chini ya sheria za enzi za ukoloni, vitendo vya ushoga ni kinyume cha sheria nchini Uganda lakini tangu uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1962 hakujawai kuhukumiwa kwa shughuli za maelewano za mapenzi ya jinsia moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.