Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

DRC: Umoja wa Afrika kuunga mkono mchakato wa Luanda Angola

NAIROBI – Umoja wa Afrika, umesema utaendelea kuunga mkono mchakato wa Nairobi na ule wa Luanda Angola, kuhusu kusaidia kupatikana kwa amani mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Mwandishi wetu Emmanuel Makundi, anafuatilia mkutano huo na hii hapa ni taarifa yake

Mkuu wa tume ya umoja wa Afrika, Musa Fakhi Mahamat
Mkuu wa tume ya umoja wa Afrika, Musa Fakhi Mahamat © Mustafa Abumunes, AFP
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 36 wa wakuu wa nchi, mkuu wa tume ya umoja huo, Musa Fakhi Mahamat, amesema ofisi yake imeweka mikakati kuhakikisha maridhiani na amani inapatikana kwenye eneo la maziwa makuu hasa mashariki mwa DRC.

Mahamati amesema kujirudia mara kwa mara kwa machafuko kwenye eneo hilo, kumeendelea kusababisha madhila kwa raia ambao ndio wahanga wakubwa, akiyataka makundi yenye silaha kusitisha mashambulio.

Matamshi yake yamekuja wakati huu, viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakijaribu kuongeza shinikizo kwa waasi wa M23 kujiondoa kwenye maeneo wanayoyashikilia, kundi hili likituhumiwa kusaidiwa na Rwanda, ambayo hata hivyo inakanusha.

Wakuu wa nchi watakaokutana mwishoni mwa juma hili, wanatarajiwa kutoa uelekeo wa kiusalama kwa bara lao, ambalo linaendelea kushuhudia mizozo inayokwamisha maendeleo ya nchi hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.