Takriban watu 5 wafariki kufuatia kuporomoka kwa jengo karibu na mji wa Nairobi
Takriban watu watano, wakiwemo watoto wawili, wamefariki dunia siku ya Jumatatu baada ya jengo la ghorofa sita kuporomoka katika mji ulio nje kidogo ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi, gavana wa mji huo amesema kulingana na shirika la habari la AFP.
Imechapishwa:
Jengo hilo lililokuwa likijengwa katika eneo la Kiambu liliporomoka Jumatatu asubuhi, Gavana Kimani Wamatangi amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter. "Tumepoteza watu watano katika jengo lililoporomoka," amesema na kuongeza kuwa juhudi za kuwatafuta na kuwaokoa wahanga zinaendelea.
Sababu za ajali hiyo hazijafahamika mara moja.
Ujenzi mbovu, kutofuata kanuni na ufisadi kumesababisha ajali kadhaa mbaya siku za nyuma nchini Kenya, chombo cha uchumi wa Afrika Mashariki, ambacho kimekuwa kikikumbwa na ongezeko la mali isiyohamishika kwa miaka kadhaa.