Pata taarifa kuu

Burundi yampata Waziri Mkuu mpya baada ya shutuma za jaribio la 'mapinduzi'

Rais wa Burundi Jenerali Évariste Ndayishimiye Jumatano asubuhi amemfuta kazi Waziri wake Mkuu, Jenerali Alain-Guillaume Bunyoni na mmoja wa watu wenye nguvu na ushawishi zaidi nchini humo, ambaye nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mkuu wa wizara kuu inayojumuisha Mambo ya Ndani, Usalama wa Umma na Maendeleo ya Jamii.

Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, Juni 13, 2020 huko Bujumbura.
Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, Juni 13, 2020 huko Bujumbura. AP - Berthier Mugiraneza
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Burundi pia alimfuta kazi mapema asubuhi mkurugenzi katika ofisi yake, Jenerali Gabriel Nizigama, ambaye nafasi yake ameteuliwa afisa mwenye cheo cha kanali kutoka idara ya upelelezi, ambaye bado kijana.

Mageuzi  haya ya uongozi wa mamlaka nchini Burundi yanatokea siku chache baada ya Rais Ndayishimiye kuwashutumu hadharani "wale wanaojiamini kuwa wana nguvu zote" na wana ndoto ya kufikia madaraka kupitia mapinduzi, kutoka wasaidizi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.