Pata taarifa kuu
UTAWALA BORA-UFISADI

Mzozo waibuka kuhusu mishahara 'mikubwa' kwa wabunge DRC

Madai ya mpinzani wa DRC juu ya mishahara ya wabunge unaokadiriwa kufikia dola 21,000 kwa mwezi kwa kila mbunge yamezua mzozo mkali siku ya Jumatano nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo idadi kubwa ya watu wanaishi kwa kutumia chini ya dola mbili kwa siku.

Wabunge wakishiriki moja ya vikao vya Bunge, Kinshasa, Agosti 19, 2019.
Wabunge wakishiriki moja ya vikao vya Bunge, Kinshasa, Agosti 19, 2019. JUNIOR D.KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Jumanne, mwanasiasa wa upinzani Martin Fayulu, ambaye anaendelea kudai ushindi wake katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2018 alioshinda Rais Félix Tshisekedi, alihakikisha kwamba "malipo ya wabunge wa kitaifa yamefikia tangu Januari 2022 hadi dola 21,000 kwa mwezi".

"Hii inaitwa rushwa kubwa, usimamizi mbaya na uporaji wa fedha za umma na mamlaka ya uporaji (ya Tshisekedi) katika kutafuta uhalali wa ndani", aliongeza, akitaka "kufutwa mara moja" kwa "ununuzi huu wa dhamiri kwa kuiba hazina ya serikali" .

"Mishahara hii mikubwa ya wabunge ni ya kuchukiza ikilinganishwa na ile madaktari, maprofesa wa vyuo vikuu au watumishi wa umma wanapata", ameshutumu Trésor Kibangula wa taasisi ya utafiti wa utawala ya "Ebuteli", yenye makao yake makuu katika Chuo Kikuu cha New York.

Mishahara ya wabunge inayodilika katika hali ya kutokuwepo na uwazi, imegawanywa katika vipengele kadhaa, kama vile "hifadhi ya bunge ya dola 3,000 hadi 3,500 zinazolipwa kwa kila mbunge" bila msingi wa kisheria, amesema.

Mtumishi wa kawaida wa umma wa Kongo anapata faranga za Kongo 155,000 (sawa na dola 52.5), profesa wa chuo kikuu anapata wastani wa dola 2,000 wakati mshahara wa daktari ni karibu dola 1,000.

Ofisi ya Bunge yakanusha madai ya mpinzani

"Hakuna mbunge wa kitaifa anayeweza kusema na kuthibitisha kwamba anapata dola 21,000, ikiwa ni pamoja na maafisa waliochaguliwa wa chama cha Ecidé", chama cha Bw. Fayulu, mbunge Samuel Mbemba, mkurugenzi katika ofisi ya  spika wa Baraza la Wawakikilishi nchini DRC amejibu kwa shirika la Habari la AFP.

"Ni hotuba ya watu wengi iliyofanywa kwa makusudi ili kuunda mzozo wa kijamii kati ya wabunge wa kitaifa na watu wanaowawakilisha na kuwasaidia", ameongeza, akimtuhumu Martin Fayulu "kufikiria" kuhusu mishahara ya wabunge.

DRC yenye utajiri wa maliasili, ni nchi ya 10 maskini zaidi duniani: 77.2% ya wakazi wake wanaishi kwa dola 1.9 kwa siku, kulingana na Umoja wa Mataifa. Ikichukuliwa kuwa mojawapo ya nchi fisadi zaidi, DRC inashika nafasi ya 169 kati ya nchi 180 kulingana na shirika la kimataifa la Transparency International.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.