Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Wanne waidhinishwa na Tume ya Uchaguzi kuwania urais mwezi Agosti

Nchini Kenya, Tume ya Uchaguzi imetagaza kuwa uchaguzi Mkuu wa mwezi wa nane, utakuwa na wagombea wanne wanaotafuta wadhifa wa urais, baada ya kumalizika kwa zoezi la mchujo.

Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, pamoja na Naibu rais William Ruto
Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, pamoja na Naibu rais William Ruto © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wagombea hao wanne waliopitishwa na Tume ya Uchaguzi ni pamoja na Naibu rais William Ruto, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na mwanasiasa mkongwe Raila Odinga, Wakili David Mwaure na Profesa George Wajackoyah.

Hii ndio idadi ndogo ya wagombea kuwahi kuidhinishwa na Tume ya Uchaguzi kuwania urais katika taifa hilo la Afrika Mashariki tangu kuanza kwa siasa za vyama vingi miaka ya tisini.

Tume ya Uchaguzi nchini humo imesema kati ya watu zaidi ya 50 waliokuwa na nia ya kuwa wagombea, ni wanne tu ndio waliofikia vigezo vinavyotakiwa ili kuwania nyadhifa hiyo ya juu.

Kwa idadi hii, kinyanganyiro kinaonekana kuwa wazi kuwa kati ya Odinga ambaye anaungwa mkono na rais Kenyatta na Ruto. Wawili hawa, wanaahidi mapinduzi ya kichumi.

Profesa Wajackoyah yeye anaahidi kupanua serikali, kupunguza siku za kufanya kazi kwa wiki kutoka tano hadi siku nne na kuhalalisha bangi.

Wakili Mwaure yeye anaahidi kupambana na ufisadi iwapo ataingia madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.