Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa urais nchini Kenya: Wagombea wa urais wailalamikia Tume ya Uchaguzi

Kampeni za uchaguzi wa urais wa Agosti 9 sasa zimepamba moto nchini Kenya. Wikendi iliyopita, tume ya uchaguzi iliidhinisha wagombea wawili wakuu, Raila Odinga na William Ruto. Lakini wiki hii kulishuhudiwa uhasama kati ya pande hizi mbili, na katikati ya madai ya kwanza ya jaribio la udanganyifu kwa upande wa William Ruto.

Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, pamoja na Naibu rais William Ruto
Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, pamoja na Naibu rais William Ruto © AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi, makamu wa rais - ambaye sasa ni mgombea katika uchaguzi huo- wakati alikuwa akiwapokea mabalozi wa Umoja wa Ulaya katika makazi yake, aliwashangaza wafuasi wake kwa kusema kuwa karibu majina milioni moja yameondolewa kwenye daftari la wapiga kura, hasa katika ngome zake na akishutumu wasaidizi wa Rais Uhuru Kenyatta kwa jaribio la udanganyifu.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alikanusha haraka na kusema kuwa ni madai yasiokuwa na msingi, na kubaini kwamba baadhi ya majina yanaweza kuhamishwa kutoka ofisi moja hadi nyingine. Aliwatoleawito Wakenya kutulia wakisubiri faili ya mwisho kuchapishwa katika Jarida Rasmi.

Kura za maoni zinatabiri kura zilizokaribiana

Mapema wiki hii, William Ruto alivikosoa vyombo kadhaa vikuu vya habari kwa kuegemea upande mwingine na kumpendelea mpinzani wake, akibaini kwamba atasusia mdahalo wa urais uliopangwa kufanyika Julai 12, 2022. Jumamosi, William Ruto alirejelea kauli yake na kusema ana "imani" na tume ya uchaguzi wakati wa kuhalalisha kugombea kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.