Pata taarifa kuu
KENYA-HAKI

Kenya : Mahakama yaamua mchakato wa marekebisho ya Katiba ni kinyume cha sheria

Mahakama ya Juu chini Kenya, imeamua kuwa mchakato wa marekebisho ya Katiba maarufu kama BBI, ulioazishwa na rais Uhuru Kenyatta ni kinyume cha Katiba. 

Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wakipeana mikono Machi 9, 2018, Nairobi, Kenya.
Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wakipeana mikono Machi 9, 2018, Nairobi, Kenya. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu, umeonekana kama pigo kwa rais Kenyatta na washrika wake, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti. 

Majaji Sita kati ya Saba wakiongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome wa  Mahakama hiyo yenye uamuzi wa mwisho nchini Kenya, wamesema rais hana uwezo kikatiba chini ya kifungu nambari 257 kuanzisha mchakato wa katiba. 

Hata hivyo, Mahakama hiyo imesema mchakato wa Marekebisho ya Katiba unaweza kuendelea kwa kutumia bunge au njia nyingine, ilimradi rais asihusishwe. 

Wakenya wamekuwa na mtazamo huu baada ya hatua ya Mahakama. 

Mchakato huo ulilenga kuifanyia marekebisho ya Kenya iliyoapatikana mwaka 2010 kwa kile Kenyatta na washirika wake kama kiongozi wa upinzani Raila Odinga walisema marekebisho hayo yangesaidia kuleta umoja wa kitaifa, suala ambalo limewagawa Wakenya kisiasa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.