Pata taarifa kuu

Hatima ya Wanyarwanda walioachiliwa huru na kupewa hifadhi Niger kujulikana

Je, Niger itaamua kuwafukuza maafisa wanane wa zamani wa serikali ya zamani ya Rwanda hadi Kigali saa chache zijazo? Mwanzoni mwa mwezi Januari, Niamey, kwa shinikizo la Umoja wa Mataifa, iliahirisha kwa siku thelathini sheria yake ya kuwafukuza mawaziri hao wa zamani na maafisa wa utawala wa Habyarimana, ambao baadhi yao wameachiliwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya Rwanda.

Picha ya zamani iliyopigwa mwaka 2014 mjini Arusha mbele ya jengo lililotumiwa kama Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR).
Picha ya zamani iliyopigwa mwaka 2014 mjini Arusha mbele ya jengo lililotumiwa kama Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR). AFP - NICHOLE SOBECKI
Matangazo ya kibiashara

Mvutano kati ya Niger na Umoja wa Mataifa, ulioanza Desemba 23, 2021, unaendelea.

Wkati huo, mamlaka nchini Niger ilifuta vibali vya kuishi nchini humo vilivyotolewa kwa Wanyarwanda wanane waliokuwa wamewasili Niamey.

Mawaziri na maofisa wa zamani chini ya utawala wa Juvénal Habyarimana, aliohudumu wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, wanne kati yao waliachiliwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), na wengine wanne kwa muda mrefu wametumikia kifungo chao.

Lakini kwa zaidi ya miaka kumi na tano, hakuna nchi iliyokubali kuwapokea watu hawa wanaokataa kurudi Rwanda kwa kuhofia kufungwa tena. Kwa miaka mingi na hadi mwanzoni mwa mwezi wa Desemba, waliishi Arusha, kwa gharama na chini ya ulinzi wa Umoja wa Mataifa. Lakini mnamo Novemba 15, Niger hatimaye ilijitolea na kutia saini makubaliano na Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT), yenye jukumu la kusimamia faili za mwisho za ICTR, iliyofungwa mwishoni mwa mwaka 2015.

Mwanzoni mwa mwezi wa Desemba, kwa msingi wa makubaliano haya, Wanyarwanda wameendelea kuishi huko Niamey. Lakini hiyo ilikuwa bila kutegemea "shinikizo la kidiplomasia" lililotolewa na Niger katika sheria yake ya kufukuzwa iliyotolewa kwa Wanyarwanda wanane wiki tatu baadaye. Kisha wana hadi Januari 3 kuondoka nchini. Kisha, kwa ombi la Umoja wa Mataifa, Niger ilikubali kuwapa Wanyarwanda hao wanane siku 30 zaidi kutafuta makao mapya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.