Pata taarifa kuu
KENYA-NjAA-WFP

Ukame wasababisha baa la njaa Kaskazini Mashariki mwa Kenya

Nchini Kenya, maeneo kadhaa hasa kaskazini mashariki mwa taifa hilo yanaendelea kumbwa na hali ya ukame kutokana na kuchelewa kwa mvua, maelfu ya raia wakiwa wameathirika.

Mkaazi wa kijiji cha Maalimin akippkea msaada wa chakula kutoka WFP, 10/01/2022
Mkaazi wa kijiji cha Maalimin akippkea msaada wa chakula kutoka WFP, 10/01/2022 © WFP/Martin Karimi
Matangazo ya kibiashara

Hillary Ingati amezuru maeneo kadhaa katika kaunti ya Garissa kilomita 328 kutoka Nairobi na kutauandalia ripoti ifutayo.

Maalmini, kilomita 54 kutoka kaunti ya Garissa, hapa raia wamefika kwa wingi kupokea chakula cha msaada kutoka kwa shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Saretho Osman Maalim ni moja wa raia waliofika hapa kupokea msaada.

“Nimepata mtama, maharagwe na pia mafuta”

 Ismael Gilmal Ahamed, Ana familia ya watu kumi, anayeleza alivyoaathirika.

“Rasilimali ya nyumba imeenda chini na hasa mifugo zimekufa alafu mvua hatujapata hapa Maalimini, Mifugo yetu imehama hadi êneo la dadaab, Ngamia yangu tatu ilikufa, ngo'mbe amebaki mmoja na mbuzi walikufa hamsini”

Kwa kipindi cha mwaka moja sasa, Eneo hili la Maalimini tunaelezwa halijapata mvua.

Daudi Elmoge ni chifu wa êneo hili.

Mtu ambaye alitoka hapa na mbuzi 1000 , alipoteza na alibaki na 180 , wengine walikuwa na 200 wamebaki na hamsini kwa hivyo watu wameathrika na mifugo yao imeishia dadaab na hata hapa hakuna matarajio ya mifugo kurudi kwa maana hakuna mvua.

 Didmas Ewaton, ni afisa wa WFP, kitengo cha Garissa.

Katika garissa kaunti, tunaangazia wanufaika 70,000 ambayo ni makaazi 11,160  hiki chakula tunatoa kila familia iliyo na watu sita na hawa watu sita wanapata gunia moja ya mtama, kilo kumi na moja ya maharagwe na kilo nne za mafuta.

Baadhi ya maduka hapa Maalimini kwa sasa yamefungwa, wafanyabiashara wakieleza kuwa hali ya ukame imesabaratisha baishara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.