Pata taarifa kuu
ETHIOPIA - USALAMA - SIASA

Ethiopia : Muuwaji wa mkuu wa jeshi ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Mahakama kuu nchini Ethiopia, imemhukumu kifungo cha maisha jela Mesfin Tigabu, baada ya kupatiakana na hatia ya kumuua aliyekuwa mkuuwa jeshi nchini humo, Seare Mekonen, Juni 22 mwaka 2019.

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, akitangaza kuwa hali ya eneo la Amhara ni jaribio la mapinduzi ya serikali.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, akitangaza kuwa hali ya eneo la Amhara ni jaribio la mapinduzi ya serikali. Ethiopian TV/AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Ethiopia iliyataja mauwaji Seare Mekonen, kuwa njama ya kuyumbisha serikali, ikituhumu  aliyekuwa  mkuu wa usalama eneo la  Amhara, Asaminew Tsige, kuwa na njama ya kuipundua serikali wakati huo.

Jaribio hilo la mapinduzi ya serikali nchini Ethiopia, lilisabisha maafisa wengine wa ngazi ya juu serikalini kufariki, akiwemo rais wa eneo la Amhara, Ambachew Mekonon, na mkuu sheria eneo hilo Migbaru kebede.

Tsige, aliyekwenda mafichoni siku chache baada ya mauwaji hayo, pia aliuawa wakati wa ufyatulianaji wa risasi siku chache baadaye.

Jaribio hilo la mapinduzi pia lilichangia serikali kukatiza mtandao nchini Ethiopia kwa siku 10, serikali ekiendesha operesheni kali eneo la Amhara na jiji kuu la Addis Ababa, kuwasaka waliokuwa wandani wa Tsige.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.