Pata taarifa kuu
SUDANI-UMOJA WA MATAIFA-UMOJA WA AFRIKA

Raia wa Darfur wapewa ulinzi zaidi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana jana alhamisi na tume ya mseto inayojumuisha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur (UNAMID) na kuitaka kuwajibika vilivyo kwa kuwalinda raia wa Jimbo hilo.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakijadili hali inayojiri katika jimbo la Darfur.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakijadili hali inayojiri katika jimbo la Darfur. REUTERS/Shannon Stapleton
Matangazo ya kibiashara

Katika azimio liliyochukuliwa kwa pamoja, baraza hilo limemtaka katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuipa tume hio ya mseto mikakati mipya, ambayo ni kulinda raia, kurahisishia usafirishaji wa misaada ya kiutu, kuunga mkono jitihada za usuluhishi kati ya Khartoum na makundi ya wapiganaji na pia kati ya jamii.

Azimio hilo linatambua kwamba tume hio ya mseto inakabiliwa na matatizo mengi, ambayo yanasababisha kutotekeleza kazi yake ipasavyo, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ushirikiano na serikali na ukosefu wa usafiri wa anga.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka tume hio ya mseto kueleza kwa kina hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa ili itekeleze mikakati mipya itakayopewa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeanza kujadili hali hio, kabla ya tume hio kubadilishiwa uwezo mwezi ogasti mwaka 2014.

Tume ya mseto inayojumuisha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfour (UNAMID) iliundwa tangu miaka sita iliyopita na ina wanajeshi na wafanyakazi wengine takriban 16.200, na ni kikosi cha pili muhimu duniani baada ya Monusco nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Lakini tume hio ya mseto inayojumuisha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika inakabiliwa na matatizo ya majukumu na uongozi, kwani maamuzi yanapaswa kuchukuliwa na taasisi hizi mbili, balozi wa Uingereza, Mark Lyall Grant, amesema katika mkutana na vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.