Pata taarifa kuu
MISRI-Uchaguzi

Abdel Fattah al-Sissi atangaza kugombea kwenye kiti cha urais nchini Misri

Mkuu wa majeshi wa Misri, Jenerali Abdeli Fattah al-Sisi ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake ya ukuu wa majeshi ili kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi ujao huku akiahidi kupambana na ugaidi iwapo atateuliwa. “Wananchi wenzangu, nimevaa kwa mara ya mwisho sare hii ya kijeshi, baada ya kuuamua kuachia ngazi kwenye wadhifa wangu wa kuliongoza jeshi na waziri wa ulinzi, kwa hio leo naachana na sare hii ya jeshi na kuendelea kutetea taifa langu”, amesema al-Sissi.

Abdel Fattah al-Sissi, akitoa tangazo la kugombea kwenye kiti cha urais kupitia televisheni, machi 26 mwaka 2014
Abdel Fattah al-Sissi, akitoa tangazo la kugombea kwenye kiti cha urais kupitia televisheni, machi 26 mwaka 2014 AFP / AL-MASRIYA TV
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Abdeli Fattah al-Sisi, ambaye amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kuipindua serikali ya Mohamed Morsi anapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti hicho kwakuwa hakuna upinzani mkubwa anaotarajiwa kuupata toka kwa wagombea wengine.

Licha ya kuungwa mkono na sehemu kubwa ya wananchi wa Misri, hatua yake ya kuamua kugombea urais kwenye uchaguzi wa mwezi June, kumeleta mgawanyiko miongoni mwa wananchi ambapo wapo wanaoona kuwa kiongozi hiyo hakupaswa kuwania kiti hicho na badala yake angebakia kwenye nafasi yake ya ukuu wa majeshi na waziri wa Ulinzi.

Tayari baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wanakosoa hatua ya al-Sisi wakisema uchaguzi hautakuwa huru na haki kwakuwa Serikali yenyewe inayoandaa uchaguzi huo haikuchaguliwa na wananchi.

Sissi ambaye amekua na cheo kikubwa katika jeshi, kwa sasa amevua cheo hico, kwani ametangaza kwamba anaachana na sare ya jeshi amayo aamekua akiivaa kwa kipindi cha miaka 44.

“Nimeitikia wito wa wananchi wa Misri, na ninatangaza kugombea kwenye kiti cha urais”, amesema Abdel Fattah al-Sisi, akibaini kwamba taifa lake linakabiliwa wakati huu na matatizo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, ugaidi, na kuingiliwa katika maumuzi yake na mataifa ya kigeni.

Sissi amesema hakubaliane na hali ya umasikini inayowakumba mamilioni ya vijana wa Misri pamoja na namna wagonjwa wanavyohudumiwa kimatibabu.

Amebaini kwamba taifa lake linategemea kwa sehemu kubwa misaada kutoka nje, lakini amewataka raia kwa ushirikiano na serikali kuzidisha juhudi.

Tarehe ya uchaguzi, haijafahamishwa, lakini uchaguzi huo unatazamiwa kufanyika kabla ya mwishoni mwa mwezi wa juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.