Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-MALAYSIA

Vipande vya vitu vinavyokisiwa kuwa vya ndege ya Malaysia vyaonekana Australia

Waziri kuu wa Australia, Tony Abbott ametangaza kuwa picha za Satelite za wataalam wa nchi yake zimeonesha vipande viwili vya vitu vinavyokisiwa kuwa vya ndege ya Malaysia iliyotoweka na zaidi ya abiria 230.

John Young, kiongozi wa mamlaka ya usalama wa majini wa Australia (AMSA), akiwa mbele ya ramani ya utafiti, mars 20 2014.REUTERS/Sean Davey
John Young, kiongozi wa mamlaka ya usalama wa majini wa Australia (AMSA), akiwa mbele ya ramani ya utafiti, mars 20 2014.REUTERS/Sean Davey REUTERS/Sean Davey
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Abbott ametoa tangazo hilo, siku chache tu baada ya meli za kivita za Australia kuanza kuitafuta ndege hiyo Kusini mwa bahari ya Hindi.

Abott ameliambia bunge kuwa ndege maalum imetumwa katika eneo hilo, kujaribu kuthibitisha ikiwa kweli vitu vilivyoonekana ni ndege hiyo ya Malaysia.

Kwa juma la pili sasa ndege hiyo iliyotoweka katika mazingira ya kutatanisha imekuwa ikitafutwa na mamlaka ya Malysia ikishirikiana na mataifa megine duniani, baharini, ardhini na hewani.

Juma lililopita China ilitoa mitambo yake kumi ya Satelite kusaidia kuitafuta ndege hiyo bila mafanikio na serikali ya Malaysia imekuwa ikitoa habari kila siku kuhusu operesheni hiyo.

Kwa sasa inasubiriwa kuthibitishwa ikiwa kweli ndege hiyo imeonekana au hapana.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.