Pata taarifa kuu

Hofu imezidi kutandaa kuhusu hatma na usalama wa Saad Gaddafi mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muamar Gaddafi

Hofu kuhusu usalama na hatma ya Saad Gaddafi mtoto wa aliyekuwa mtawala wa Libya, marehemu kanali Muamar Gaddafi imekuwa ni sintofahamu kufuatia tuhuma za mateso wanayofanyiwa wafausi wa kiongozi huyo walioko kizuizini.

Saad Gaddafi mtoto wa hayati Kanali Muamar Gaddadi
Saad Gaddafi mtoto wa hayati Kanali Muamar Gaddadi
Matangazo ya kibiashara

Hofu hii inakuja mara baada ya utawala wa Niger kutangaza kumkabidhi kwa mamlaka za Libya, mtoto wa marehemu kanali Gaddafi, Saadi Gaddafi aliyekuwa akiishi uhamishoni toka kuangushwa kwa utawala wa baba yake.

Kikosi cha wanajeshi ambako mtoto huyo anashikiliwa mjini Tripoli, kimechapisha picha kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook zikimuonesha mmoja wa askari hao akimnyoa nywele kwa nguvu Saad Gaddafi huku akiwa amepiga magoti.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameonya kuhusu vitendo wanavyofanyiwa waliokuwa wafuasi wa utawala wa kanali Gaddafi na kwamba huedna mtoto huyu akawa miongoni mwa wahanga wa mateso yanayotekelezwa na askari wa Serikali.

Saad Gadafi mwenye umiri wa miaka 40 hivi sasa alikuwa mmoja kati ya watoto wa Gadafi waliokuwa karibu na baba yake na ndie aliyekuwa akiongoza hata chama cha soka nchini Libyawakati wote wa utawala wea Marehemu Gaddafi.

Ofisi ya mwendesha mjini Tripoli imesema kuwa, Saad atashtakiwa kwa misingi ya sheria za kimataifa na anakabiliwa na tuhuma za kumsadia baba yake kusalia madarakni kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.