Pata taarifa kuu
Marekani-diplomasia

Marekani yaomba radhi Umoja wa Ulaya kufuatia matamshi makali ya waziri wake wa mambo yanje anayehusika na maswala ya Ulaya

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayehusika na maswala ya Ulaya Victoria Nuland ameomba radhi kwa Umoja wa Ulaya baada ya kutowa matamshi ambayo sio ya kidiplomasia kwa Umoja wa ulaya kuhusu mzozo unaoendelea nchini Ukraine.

rais wa Ukraine Viktor Ianoukovitch (G) akimpokea alhamisi februar 6 Victoria Nuland. jijini Kiev
rais wa Ukraine Viktor Ianoukovitch (G) akimpokea alhamisi februar 6 Victoria Nuland. jijini Kiev REUTERS/Mikhailo Markiv/Presidential Press Service/Handout via R
Matangazo ya kibiashara

Katika mawasiliano ya simu yaliowekwa mwenye mtandao wa kijamii wa Youtube Victoria Nuland anasikika akitowa kauli chafu ya kashfa na kebehi dhidi ya Umoja wa Ulaya, katika mazungumzo yake na mtu anaesadikiwa kua balozi wa marekani nchini Ukraine, Geoffrey Pyatt , jambo ambalo halikupokelewa vizuri na viongozi wa umoja wa Ulaya.

Msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni ya Marekani, Jennifer Psaki hakukanusha ukweli wa maongezi kati ya wanadiplomasia aho wawili wqa Marekani, lakini asmejizuia kutoa taarifa yoyote kuhusu “maongezi hayo ya kibinafsi kati ya wanadiplomasia hao”.

Psaki amethibitisha kwamba hana taarifa kuhusu wapi habari hio ilitolewa na kuwekwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, lakini amewatuhumu viongozi wa Urusi kwa kuchukulia habari hio na kuifanya kama matangazo, akisema kwamba njama za urusi “zimekwenda kombo”.

Psaki amesema tayari Nuland ameomba radhi kuhusu tukio hilo, lakini pia anaituhumu Urusi kuhusika katika tukio hilo.
Urusi haikubaliani na Marekani na Ubelgiji kwa mzozo unaoendelea nchini Ukaine.
Kwa upande wake msemaji wa ikulu ya Marekani, Jay Carney, amebaini kwamba hatua ya serikali ya Urusi ya “kupeperusha matangazo kwenye mtandao wa kijamii wa Twiter, ni dhahiri kwamba ina malengo fulani katika mzozo huo unaoendelea nchini Ukraine”.

“Tunashirikiana kwa kazi zetu na Umoja wa Ulaya pamona na wawakilishi wake, na hivo ndivyo alivyofanya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayehusika na maswala ya Ulaya Victoria Nuland”, ameseama Psaki. Victoria Nuland “ alikua na mazungumzo na mjumbe wa Umoja wa Ulaya anehusika na maswala ya kigeni, Catherine Ashton, amekua akiongea pia na wsenzake wa Ulaya, na kwa kweli ameomba radhi (...) kuhusu tukio hilo liliyotokea”, amesema Jennifer Psaki.

Bi Nuland kwa sasa yuko ziarani mjini Kiev, na amejitoklea mwenyewe tangu majuma yaliyopita katika kutafuta suluhu kwa mgogoro unaoendelea nchini Ukraine kati ya utawala na upinzani, na awali mwezi desemba alikutana na kwa mazungumzo na waandamanaji wanaounga mkono ushirikiano wa Ukraine na Umoja wa Ulaya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.