Pata taarifa kuu
UKRAINE-Maandamano

Mazungumzo kati ya rais wa Ukraine na upinzani yamekwenda kombo

Hali ya usalama inaendelea kuzorota mjini Kiev nchini Ukraine, kufuatia maandamano yaliyoitishwa na upinzani, ukimtaka rais Viktor Yanukovich, ajiuzulu. Mazungumzo kati ya viongozi wa upinzani na wale wa Serikali ya Ukraine, yamegonga mwamba kwa mara nyingine huku kila upande ukiendelea kusisitiza kutotekeleza matakwa ya upande mwingine.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Viongozi watatu wa vyama vikuu vya upinzani nchini humo walikuwa na mazungumzo na rais Viktor Yanukovich hapo jana, mazungumzo ambayo hata hivyo baadae viongozi hao walikabiliwa na wakati mgumu pale waandamanaji walipokataa yale waliyokubaliana na rais Yanukovich.

Vitaly Klitchko ni kiongozi wa upinzani bungeni ambaye alishiriki mazungumzo hayo, na anasema iwapo wananchi wamekataa wao pia hawana budi kuwaunga mkono.

“Vurugu zimesimama toka saa moja iliopita kwenye mtaa wa Zesco, na ni mwanzo mzuri utakao pelekea kuanza kwa mazungumzo, na nina uhakika tutafanikiwa, lakini mamlaka inatakiwa kuandaa mara moja unyanyasaji dhidi ya wanaharakati, na waliyokamatwa waachiwe. Kwa hivyo yote haya ni msingi wa kusema tuwe na mazungumzo fika”, amesema Vitaly.

Wakati huohuo, waziri mkuu wa Ujerumani Angela Merkel amempigia simu mwezaki wa Ukraine, akimtaka afute hatua iliyochukuliwa hivi karibuni na serikali ya kupinga watu kuandamana.

Hayo yakijiri, waziri wa mashauri ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius, amemuitisha balozi wa Ukraine nchini Ufaransa ili aje ajieleze kuhusu hali inayojiri nchini mwake.
Katika hatua nyingine serikali imeomba radhi kutokana na vitendo vya udhalilishaji wanavyofanyiwa baadhi ya waandamanaji wanapokamatwa na polisi.

Awali, upinzani nchini Ukraine ulitoa saa ishirini na nne kwa utawala wa nchi hiyo kuitisha uchaguzi mkuu, ama nchi hiyo ijiandae kwa maandamano makubwa zaidi.

Kauli ya upinzani ilitolewa saa chache baada ya viongozi wake kuwa na mazungumzo na raia wao, na kumtaka rais Viktor Yanukovich kuitisha uchaguzi mkuu mwingine ili kunusuru taifa hilo kutumbukia kwenye machafuko zaidi.

Waziri mkuu wa taifa hilo, aliesisitiza juzi kuwa kile kinanchofanywa na upinzani kinaenda kinyume na matakwa ya katiba ya nchi hiyo ingawa alikiri kuwa serikali yake huenda ikatekeleza matakwa ya upinzani kuitisha uchaguzi mwingine.

Rais wa Ukraine Viktor Ianoukovitch aliwatolea wito wananchi wake juzi kutoshirikiana na wabaguzi wanaochochea machafuko katika mji mkuu wa taifa hilo wa Kiev yaliosababisha vifo vya watu zaidi ya wanne.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.