Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Siasa

Rais mpya wa Jamhuri ya Afrika ya Kati anatazamiwa kuapishwa

Rais mpya wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya kati, Catherine Samba-Panza anasubiriwa kuapishwa leo mjini Bangui. Sherehe hizo zitahudhuriwa na viongozi kutoka mataifa mbalimbali. Bi Catherine Samba-Panza amechukua wadhifa huo kwa kuteuliwa hivi karibuni na wabunge, baada ya aliekua rais wa nchi hio Michel Djotodia kulazimishwa na Jumuiya ya Kimataifa kuachia madaraka kutokana na hali ya usalama iliyokua ikiendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Catherine Samba-Panza rais mpya wa jamhuri ya Afrika ya kati
Catherine Samba-Panza rais mpya wa jamhuri ya Afrika ya kati RFI
Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo Umoja wa mataifa UN umetoa wito kwa viongozi wa mataifa ya Afrika Kuongeza wanajeshi zaidi wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati ili kulinda raia na kuzuia kile ambacho wataalamu wameonya kuwa huenda taifa hilo likakumbwa na mauaji ya halaiki.

Ni wanajeshi elfu 4 pekee wa Umoja wa Afrika ambao wako nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kati ya wanajeshi elfu 6 ambao mataifa ya Afrika yaliahidi kupeleka wanajeshi wao huku nchi ya Ufaransa yenyewe ikiwa na wanajeshi elfu 1 na 500.

Kauli ya Umoja wa Mataifa inatolewa wakati huu ambapo watu 10 wameripotiwa kuuawa jana kwenye shambulio la ulipizaji kisasi mjini Bangui.

Waziri wa mawasiliano wa nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, Adrien Pousson amesema kuwa nchi yake itahudhuria mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa mjini Roma kwa lengo la kufikia maridhiano ya kitaifa.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa ni lazima rais mpya aweke mazingira mazuri ambayo yataondoa mgawanyiko wa kisiasa kwenye taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.