Pata taarifa kuu
JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI-Siasa-Usalama

Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati akanusha madai ya kujiuzulu

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia anaelekea kujiuzulu kutokana na kuendelea kwa machafuko katika taifa lake. Ripoti kutoka Bangui zinasema kuwa rais huyo aliyemwondoa kwa nguvu rais wa zamani, Francois Bozize amekuwa akipata shinikizo kuondoka madarakani kwa kile kinachoelezwa kua anasalia kuwa kikwazo cha upatikanaji wa amani katika nchi hiyo.

REUTERS/Andreea Campeanu
Matangazo ya kibiashara

Leo Alhamisi, rais Djotodia atakuwa jijini Djamena nchini Chad kuhudhuria kikao cha viongozi wa ukanda wa Afrika ya Kati kujadili kuendelea kudorora kwa hali ya usalama katika taifa lake, na haijabainika ikiwa atatangaza kuachia ngazi.

Hata hivyo, Msemaji wa rais Djotodia, Guy Simplice Kodégué amekanusha madai hayo na badala yake kuzungumzia azma ya viongozi hao kutaka kumaliza mgogoro uliopo.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaona kuwa mkutano huo ni fursa kwa viongozi wa Afrika kuchua hatua badala ya kuiachia nchi ya ukoloni ya Ufaransa.

Katika hatua nyingine, Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu Laki Moja wanatafuta hifadhi jijini Bangui baada ya kukimbia makwao kutokana na makabiliano kati ya Wakisrito na Waislamu.

UN imeonya kuwa hali ya kibinadamu itaendelea kuwa mbaya katika taifa hilo ikiwa mapigano hayatasitishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.