Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-Mazungumzo

Afisa wa ngazi ya juu jeshini nchini Sudan Kusini auawa na mazungumzo ya kusaka amani yachelewa kuanza

Jenerali wa jeshi la nchini Sudan Kusini aliekua akiongoza kikosi kinachopambana na waasi, ameuawa katika mji wa Bor, baada ya kushambuliwa na waasi huku milio ya risaisi ikisikika mjini Juba. Mapigano yanaendelea katika mji huo wa jimbo la Jonglei kipindi hiki mazungumzo ya amani kati ya waasi na serikali yakikwama mjini Addis Ababa Ethiopia kujaribu kupata suluhu ya kudumu.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la serikali Philip Aguer anasema jeshi linakaribia kuuchukua mji wa Bor, huku msemaji wa waasi hao Moses Ruai, naye akisema wanaelekea jijini juba.
Serikali ya Juba inasema itaendelea kupambana na waasi hadi pale ushindi utakapatikana na haitawachilia huru viongozi wa waasi wanaozuiliwa.

Leo Jumatatu rais wa Sudan Omar Al Bashir atazuru Juba kuzungumza na mwenzake Slava Kiir kuhusu mzozo huu.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mazungumzo hayo juzi jumamosi, Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Tedros Adhanam, alisema Sudani Kusini inahitaji amani na maendeleo na sio vita kama inavyoshuhudiwa hivi sasa, na amewataka wajumbe wa pande zote kuhakikisha wanatumia nafasi ya mazungumzo kwa umakini ili kuhakikisha suluhu inapatikana.

Awali mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton alipongeza hatua ya pande zote kukubali kwenda katika meza ya majadiliano na ameziomba pande zote kujiepusha na kauli za kichochezi ambazo huenda zikavuruga mchakato huo.

Machafuko hayo yamesababisha watu zaidi ya laki mbili kuyakimbia makazi yao na watu zaidi ya elfu moja wamepoteza toka mapigano hayo yalipoanza katikati ya mwezi Desemba mwaka jana.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.