Pata taarifa kuu
JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

Milio ya risasi za rashasha yasikika mjini Bangui

Wanajeshi wa Ufaransa wameonekana wengi katika mitaa ya mji wa Bangui ambapo milio ya risasi imesikika leo ijumaa na kusabaisha hofu kwa hali inayojiri wakati huu katika mji huo, huku machafuko yakiendelea kuongezeka.Shirika la Msalaba Mwekundu bado halina na idadi kamili , lakini baadhi ya taarifa zinafahamisha kwamba maalfu ya watu wameuwawa na risasi au kumchomwa visu na mapanga, tangu machafuko hayo yalipoanza.

Matangazo ya kibiashara

Tangu wanajeshi wa Ufaransa waingiliye kati, makabilianao ya kidini kati ya kundi la wanamgambo wa kikristo “ Anti-balaka”ns waasi wa zamani wa kundi la Séléka, ambao wengi wao ni waislamu,waliyomuondoa madarakani rais François Bozizé mwezi machi mwaka 2013. .

Wakristo wengi , ambao ni waathirika wakati waasi wa Seleka walipokua wakiendesha mauwji dhidi yao, wana kiu cha kulipiza kisasi dhidi ya waasi hao wa zamani na raia wa kawaida kutoka jamii ya waislamu, ambao wanahusishwa na waasi wa Seleka.

Kila siku idadi ya vifo huongezeka. Usiku wa alhamisi hadi leo ijumaa, wanajeshi wawili wa kikosi cha umoja wa Afrika ( Misca ) kutoka Jamuhuri ya kidemokrasia ya Ccongo waliuawa katika makabiliano ya risase.

Wanajeshi wa Tchad ambao wamepiga kambi mjini Bangui wakiwa na silaha za kutosha, wanawalindia usalama waislamu ambao ni wachache pamoja na kutoa ulinzi wa rais Michel Djotodia, ambae ni kiongozi wa zamani wa waasi wa Seleka.

Ijumaa asubuhi, raia angalau mmoja ameuawa na watoto kadhaa wamejeruhiwa na gruneti iliyorushwa na askari wa Chad ambao walikuwa wakilinda msafara wa raia kutoka Chad, ambao walikua wakikimbia mji kutokana na matusi yaliyo kua yakitolewa dhidi yao na umati wa watu waliokusanyika kando ya barabara.

Katika usiku wa jana kuamkia leo, milio ya risasi ilisikika katika maeneo ya karibu na ikulu ya rais wa mpito Michel Djotodi.

Mji wa Bangui unakabiliwa na chuki ya kidini.

Msemaji wa rais Guy-Simplice Kodegue , amesema risasi hizo zimefyatuliwa baada ya hali ya kutokuelewana kujitokeza kati ya wanajeshi wa kikosi cha umoja wa Afrika ( Misca ) waliyoko karibu na ikulu na majeshi ya Seleka .

Miili arobaini ilikusanywa katika mji tangu Jumatano , kwa mujibu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC), miili sitini ilipatikana pia Jumatatu katika mji mkuu, hayo yamethibitishwa na msemaji wa ICRC.

Kulingana na Ofisi ya Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), vurugu hizo zimesababisha raia wanayahama makaazi yao.

Takribanai raia laki 7 na alfu 10 wameyakimbia makaazi yao, ikiwa ni pamoja na laki 2 na alfu 14 kwa jumla ya laki 8 mjini Bangui.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.