Pata taarifa kuu
JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

Viongoi wakuu nchini jamuhuri ya Afrika ya Kati akiwemo Rais Djotodia wawatolea raia wito wa kudumisha amani nchini humo

Rais wa kipindi cha mpito nchini Jamhuri ya Afrika ya kati Michel Djotodia pamoja na viongozi wa kidini wameendelea kuwatolea wito wananchi wa taifa hilo wa kuachana na mauaji na badala yake kupendana na kuepusha tofauti zao za kidini na kuendelea kueshi kwa ushirikiano kama ilivyokuwa miaka ya hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Rais Djotodia ametumia fursa ya kukemea matamshi ya Mshauri wake na kiongozi wa zamani wa waasi wa seleka Abakar Sabone ya kutaka kuigawa nchi hiyo katika sehemu mbili moja kwa wakristo na nyingine kwa waislam.

Akizungumza jijini Bangui, Djotodia amesema pendekezo la mshauri wake ni la kupotosha na atamchukulia hatua za kisheria.

Djotodia amesema Abakar Sabone ametoa kauli hiyo kama yeye, na kauli hio inamuhusu mwenyewe, tabia kama hiyo inahitaji kuchukuliwa hatua kali za kisheria, ili iwe mfano kwa watu ambao hawajali kitu na wasiowajibika. Tabia hii haikubaliki kwa kiongozi wa ngazi ya juu kama Sabone.

Viongozi wa dini nchini humo wanasema wanashangaa kuona watu wanaotumia dini ya Kikiristo na Kislamu kuendelea kuchochea machafuko nchini humo.

Dieudonné Nzapalanga Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki mjini Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, amewatolea wito waumini wote wa dini mbalimbali nchini nchini humo kutofuata kauli potovu zinazotolewa na baadhi ya viongozi, na kuwataka wadumishe mshikamano, akisema kwamba hata yeye kwa sasa anaishi kwenye makao makuu ya Kanisa Katoliki na Kiongozi wa Jumuiya ya waislamu nchini humo.

Wananchi wa Afrika ya Kati wanakabiliwa na ukosefu wa usalama na maelfu wamekimbia makwao, kipindi hiki majeshi ya Ufaransa na yale ya Umoja wa Afrika yakiendeleza Opereshenii ya kuwapokonya silaha makundi ya wapiganaji na kulinda amani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.