Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Mashirika yanayotetea haki za kibinadamu yaomba Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati mzozo unaoendelea kuibuka Jamuhuri Afrika ya Kati ili kukomesha mauwaji yanayoendelea nchini humo

Shirika la Kimataifa la Kutetea haki za Binadamu la Amnesty International linasema kuwa kundi la waasi wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati liliwaua watu 1,000 kwa kipindi cha siku mbili mwezi huu.Shirika hilo linasema kuwa kwa sasa kinachoendelea nchini humo ni ukiuwakji wa haki za Binadamu.

Matangazo ya kibiashara

Shirika lingine la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch nalo linasema kuwa wakati umefika kwa Umoja wa Mataifa kutuma majeshi ya kulinda amani nchini humo.

Mbali na hayo kikosi cha Umoja wa Afrika nchini humo FOMAC kinasema kuwa kinakabiliwa na idadi ndogo ya wanajeshi katika Oparesheni ya kulinda amani nchini humo.

Mwishoni mwa juma liliyopita,rais wa nchi hio Michel Djotodia, aliwafuta kazi kwa pamoja mawaziri watatu pamoja na mkurugenzi wa hazina, bila hata hivo kuomba ushauri waziri mkuu Nicolas Tiangaye, kama jinsi inavyoeleza katiba ya serikali ya mpito ya nchi hio.

Viongozi hao wawili pamoja na rais wa baraza la kitaifa la mpito,Ferdinand Nguendet, walikutana kwa mazungumzo hivi karibuni, ili kupatia ufumbuzi hali ya kutoelewana inayojitokeza kati yao, na waliafikiana kukomesha uhasama huo.

Michel Djotodia na Nicolas Tiangaye wameafikiana kufanya mabadiliko kwenye serikali, huku kukipewa kipao mbele kwenye serikali hio usawa kulingana na nguvu za vyama vya siasa vinavyo sajiliwa nchini humo.

Waziri mkuu Nicolas Tiangaye amesema mazungumzu yanahitajika ili kukwamua hali hio anayoendelea nhini Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.