Pata taarifa kuu
Thailand

Waandamanaji nchini Thailand wazingira ofisi ya wizara ya fedha kupinga muswada wa waziri mkuu bungeni

Maelfu ya waandamanaji nchini Thailand  wanaopinga serikali ya waziri mkuu Yingluck Shinawatra, hii leo wamezizunguka ofisi za wizara ya fedha nchini humo na kuahidi kuzingira ofisi zaidi za serikali kushinikiza kujiuzulu kwa waziri Shinawatra. 

Waandamanaji nchini Thailand wakiwa tayari kupambana na polisi mjni Bangkok
Waandamanaji nchini Thailand wakiwa tayari kupambana na polisi mjni Bangkok REUTERS/Damir Sagolj
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo dhidi ya waziri mkuu Yingluck na kaka yake aliyewahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Thaksin Shinawatra, ni makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu mwaka 2010 wakati utawala wa kifalme ulipokabiliwa na maandamano kama haya ambapo raia zaidi ya 90 waliuawa.

Waandamanaji hao wanaokadiriwa kufikia elfu tau wameandamana kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Bangkok wakishinikiza kujiuzulu kwa waziri mkuu Yingluck kwa madai kuwa kiongozi huyo amewsilisha bungeni muswada unaolenga kumfutia hatia kaka yake Thaksin Shinawatra anayeishi uhamishoni.

Maandamano haya yamezusha hofu ya kuzuka machafuko zaidi kwenye mitaa na hata nchi nzima kama ilivyoshuhudiwa mara baada ya mapinduzi ya kuung'oa utawala wa waziri mkuu Thaksin Shinawatra mwaka 2006.

Waandamanaji hao wanataka jeshi la nchi hiyo liingilie kati hali hiyo na kuhakikisha Shinawatra harejei nchini humo wakimtuhumu kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka wakati wa utawala wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.