Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Wanasheria nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati waanza mgomo kupinga mauaji ya mwenzao

Wanasheria nchini Jamhuri ya Afrika ya kati wametangaza kuanza mgomo utakaodumu kwa muda wa mwezi mmoja ili kupinga mauaji ya kikatili ya Mwanasheria mwenzao Modest Bria mwishoni mwa juma lililopita. Uamuzi huo ulitangazwa baada ya mkutano mkuu wa Wanasheria uliofanyika jana jumatau katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.

AFP PHOTO / PACOME PABANDJI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Waziri wa Usalama wa Jamhuri ya Afrika ya kati, Joshua Binoua, Hakimu Modest Bria pamoja na msaidizi wake waliuawa jumamosi usiku mjini Bangui na watu wenye silaha waliobainishwa na serikali kuwa ni waasi wa zamani wa kundi la Seleka kama anavyobainisha.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki -moon ametoa pendekezo kwenye Baraza la Usalama la Umoja huo UNSC kupeleka askari wapatao 9,000 kulinda amani kulingana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.

Katika ripoti yake, Ban pia ametoa onyo juu ya kuongezeka kwa ghasia baina ya waislamu na wakristo, ambapo pia ametoa wito kwa UNSC kuchukua hatua za haraka juu ya mzozo huo.

Waasi wa Seleka walifanikiwa kuagusha utawala wa Francois Bozize mwezi Machi mwaka huu, hata hivyo serikali ya mpito inayoongozwa na Michel Djotodia nayo haijajizolea umaarufu kutokana na kushindwa kutatua matatizo ya wananchi wa Taifa hilo wapatao milioni 4.5.

Wanadiplomasia wanasema hivi karibuni Ufaransa inatarajiwa kupendekeza jinsi majeshi ya Afrika yatakavyoweza kusaidia kuimarisha usalama nchini humo, hatua ambayo inatarajiwa kuzindua uundwaji wa kikosi cha kulinda amani kitakachoingia nchini humo mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.