Pata taarifa kuu
UJERUMANI-ujasusi

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel agadhabishwa na tuhuma za Marekani kuchunguza mawasiliano yake ya simu

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amempigia simu rais wa Marekani Barack Obama, baada ya kupokea taarifa kuwa serikali ya Marekani imekuwa ikichunguza mawasiliano yake ya simu.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amempigia simu raisi wa Marekani Barack Obama kuitaka Marekani itoe maelezo ya tuhuma za kuchunguza simu yake
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amempigia simu raisi wa Marekani Barack Obama kuitaka Marekani itoe maelezo ya tuhuma za kuchunguza simu yake www.tvnz.nz
Matangazo ya kibiashara

Merkel amesema kuwa kama kweli Marekani imekuwa ikifanya hivyo, basi ni suala ambalo halikubaliki kamwe na anataka maelezo ya kina.

Hata hivyo Ikulu ya Marekani inasema kuwa rais Obama amemwambia Kansela Merkel kuwa Marekani haijachunguza mawasiliano yake.

Mapema juma hili rais wa Ufaransa Francois Hollande alighadhabishwa na taarifa kuwa Marekani imekuwa ikisikiliza mawasiliano ya Mamilioni ya raia wa Ufaransa tuhuma ambazo Marekani imekanusha.

Naye Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius alitoa agizo kwa Balozi wa Marekani nchini humo kupitia katika Wizara ya Mambo ya nje kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo.
Aidha waziri mkuu wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault ameeleza kushangazwa na kitendo kilichofanywa na Marekani kwa kuona ni makosa kuingilia masuala binafsi ya mawasiliano ya nchi yake pasipo kuwa na sababu za kuridhisha.

Mapema jumatano Afisa mwandamizi wa ujasusi nchini Marekani James Clapper alitupilia mbali kuwa Washington imekuwa ikichunguza mawasiliano ya simu ya raia wa Ufaransa na kuongeza kuwa hatajadili maelezo zaidi juu ya shughuli zao kwani wanafanya ujasusi kama unaofanywa na mataifa yote kwa maslani yao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.