Pata taarifa kuu
LIBYA

Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeidan aachiliwa huru

Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeidan ameachiliwa huru baada ya kushikiliwa na waasi waliomteka Alhamisi usiku akiwa hotelini na kupelekwa kusikojulikana.

Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo la waasi lilijitokeza na kusema kuwa kiongozi huyo alikuwa  salama na katika hali nzuri ya kiafya.

Kundi hilo ambalo lina uhusiano na serikali ya Tripoli lilidai kuwa lilimshikilia Waziri Mkuu huyo katika Wizara ya Mambo ya ndani kutokana na hati ya kukamatwa kwake kwa tuhma za ufisadi, madai ambayo serikali ilikanusha.

Zeidan alitekwa usiku wa Alhamisi akiwa kwenye Hoteli ya Corinthia jijini Tripoli na watu wenye silaha ambao walitokomea naye kusikojulikana huku walinzi wake wakishindwa kumkomboa kutoka kwenye makucha ya watu hao.

Awali, Serikali ya Tripoli ilithibitsha Alhamisi asubuhi kutekwa kwa Zeidan na kusema hakuna taarifa rasmi zilizothibitsha watekaji ni kina nani na wametekeleza tukio hilo wakiwa na malengo gani.

Serikali ya Libya imesema inamshikilia mlinzi mmoja wa Waziri Mkuu Zeidan wakimhusisha na kushirikiana na watu hao wenye silaha waliomteka Kiongozi huyo akiwa Hotelini.

Aidha, taarifa ya serikali zimeeleza kuwa wanahisi watu waliohusika kwenye tukio hilo la utekaji wa Waziri Mkuu Zeidan limefanywa na waasi wa zamani na waliokuwa wanauunga mkono Utawala wa Kiongozi aliyeuawa Marehemu Kanali Muammar Gaddafi.

Mwezi uliopita Zeidan alikuwa nchini Uingereza kuomba usaidizi wa London kusaidia kukabiliana na makundi ya watu wanaoendelea kumiliki silaha  baada ya kuangushwa kwa utawala wa Gaddafi.

Mapema wiki hii,  kiongozi huyo wa serikali ya Tripoli alinukuliwa akishtumu serikali ya Marekani kwa kufanya Oparesheni nchini humo bila ya kumfahamisha na kumkamata mshukiwa wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda Anas al-Liby anayetuhumiwa kuongoza mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.