Pata taarifa kuu
MAREKANI-ISRAELI-IRAN

Serikali ya Iran yaionya Marekani kuwa waaminifu kwenye harakati za kushughulikia mpango wa nyuklia wa Taifa hilo

Serikali ya Iran imetoa onyo kali kwa Rais wa Marekani Barack Obama kuhakikisha anakuwa na msimamo juu ya kuweka imani kwa mpango wa nyuklia wa Tehran kutokana na wao kuwa tayari kuhakikisha suala hilo linatafutiwa sulu na kuachana na kusikiliza uzushi unaosambazwa na Israeli. Uamuzi wa Iran kutoa onyo hilo umekuja baada ya kufanyika kwa mazungumzo ya faragha baina ya Rais Obama na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aliyeitaka Marekani kutolegeza vikwazo vyake kwa Tehran kwa kile ambacho wamesema nchi hiyo bado ni hatari.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ndiye ametoa onyo kwa Rais Barack Obama
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ndiye ametoa onyo kwa Rais Barack Obama REUTERS/Eric Thayer
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ametaka Marekani na rais Obama kuhakikisha inaonesha uaminifu kwenye kitu ambacho Tehran imeamua kukifanya kwa kutoa ushirikiano kwa Jumuiya ya Kimataifa wakiamini ni sehemu ya kupata suluhu juu ya mpango wao wa nyuklia.

Zarif amesisitiza iwapo Rais Obama hatokuwa na imani na nchi yao kutokana na kusikiliza uzushi aliyoambiwa na Waziri Mkuu wa Israeli Netanyahu atakuwa amefanya kosa kubwa kwa kuwa juhudi zote ambazo zimeanzishwa zitakuwa zimepotea.

Waziri Zarif amesema suluhu ya kudumu kwenye mpango wa nyuklia wa Iran itapatikana kwenye meza ya mazungumzo lakini kama kutakuwa na matumizi mengine yoyote ya kijeshi yatakwamisha juhudi zinazoendelea.

Zarif amesisitiza Iran haina silaha zozote za nyuklia ambazo wametengeneza kitu ambacho kimekuwa kikisambazwa na Israel ya kwamba nchi hiyo imekuwa na mabomu ya nyuklia waliyotengeza.

Waziri huyo amemshutumu vikali Netanyahu ya kwamba amekuwa akifanya kila linalowezekana ili kuipaka matope nchi yao na kuonekana inafanya vitendo ambavyo si vya kweli.

Zarif ametaka kuwa na uwazi juu ya kile ambacho kimeanzishwa na Marekani katika kuhakikisha wanabaini kinachofanywa kwenye mpango wa nyuklia wa Iran badala ya kuendelea kutolewa taarifa za upotoshaji.

Marekani na Iran kwa mara ya kwanza zilirejea kwenye meza ya mazungumzo baada ya rais Hassan Rouhani kuzungumza na Rais Obama na kueleza hatua ya Taifa lake kuwa tayari kutoa ushirikiano kwa Jumuiya ya Kimataifa inayotaka kufanya uchunguzi juu ya mpango wao wa nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.