Pata taarifa kuu
MAREKANI-YEMEN

Alqaeda yashambulia na kuua wanajeshi 56 Yemen

Takribani Wanajeshi 56 na polisi wamepoteza maisha katika wimbi la mashambulizi yaliyotekelezwa na Wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al Qaeda nchini Yemen ambapo siku ya ijumaa iliweka alama kwa majeshi ya usalama nchini humo tangu kutikiswa kwa ngome za magaidi hao mwaka jana.

Baadhi ya wanajeshi wa Yemen ambao wamekuwa wakikabiliana na kundi la kigaidi la Al Qaeda.
Baadhi ya wanajeshi wa Yemen ambao wamekuwa wakikabiliana na kundi la kigaidi la Al Qaeda. alarabiya.net
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya wapiganaji wa Al Qaeda yalitekelezwa katika jimbo la kusini mwa Shabwa, ambapo ni ngome ya Al-Qaeda iliyozoea mashambulizi ya mara kwa mara ya Marekani kulenga wapiganaji hao.

Viongozi wa kijeshi na serikali wamesema kulikuwa na mashambulizi manne ikiwa ni pamoja na lile la kwenye kituo muhimu cha gesi.

Mashambulizi hayo ya Al Qaeda yanajiri mwezi mmoja baaada ya maafisa nchini humo kusema mipango ya alqaeada kushambulia vituo vya mafuta na gesi imedhibitiwa na wana usalama baada ya kuvuja kwa taarifa hizo za mkuu wa wapiganaji hao Ayman al-Zawahiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.