Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-G20

Mgogoro wa Syria waibua mvutano ndani ya mkutano wa G20, Marekani yazidi kusaka uungwaji mkono

Mataifa yenye nguvu za kiviwanda duniani, G20 yameendelea na mjadala mkali juu ya mzozo wa Syria na kushindwa kufikia maafikiano ya pamoja juu ya shinikizo la Marekani kuungwa mkono katika uvamizi wa kijeshi nchini Syria.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Marekani imekua ikishinikiza kuungwa mkono kuingia kijeshi nchini Syria kufuatia madai ya majeshi ya serikali hiyo kuwa yalitumia silaha za kemikali dhidi ya Syria.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema mwakilishi wa pamoja wa Umoja huo na nchi za kiarabu katika suala la Syria Lakhdar Brahimi anaelekea Urusi kuangalia jinsi ya kuweka ushawishi mpya ili mkutano wa pili kuhusu Syria uweze kufanyika.

wakati huu ambapo dunia inajikita juu ya hofu ya matumizi ya silaha za kemikali huko Syria, Brahimi atasaidia kushinikiza kufanyika kwa mkutano huo wa Geneva.

Brahimi amesema suluhu la kisiasa ndio njia pekee ya kumaliza umwagaji damu nchini Syria.

Wakati mvutano juu ya mzozo wa Syria ukiendelea Rais wa Umoja wa Ulaya Van Rompuy sanjari na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon wamesema hakuna suluhu kupitia mashambulizi ya kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.