Pata taarifa kuu
DRC-M23-ICGLR

Viongozi wa Maziwa Makuu wakutana Uganda kujadili DRC, M23 watoa onyo

Viongozi wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, ICGLR wanakutana leo jijini Kampala nchini Uganda katika kikao cha dharura kujadili hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Kikao hicho kinakuja wakati kukiwa na hali ya taharuki katika mpaka baina ya Rwanda na DRC ambapo mapigano yamekuwa yakishuhudiwa huko Goma baina wapiganaji waasi wa kundi la M23 na majeshi ya serikali ya FARDC yakisaidiwa na yale ya Umoja wa mataifa.

Wachambuzi wa maswala ya siasa wanasema hakuna mautumaini yoyote yatakayo tokea katika kikao hicho kwani si mara ya kwanza viongozi hao wanakutana hatua zinazochukuliwa.

Wakati huohuo waasi wa M23 nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wametangaza hali ya hatari katika maeneo wanayoyadhibiti, vikosi vya kulinda amani nchini humo vimeeleza,vikisema kuwa hatua hiyo haikubaliki.

Msemaji wa vikosi vya kulinda amani, nchini humo, MONUSCO, Felix Basse amesema vikosi vya kulinda amani vya umoja wa Mataifa vimekuwa vikifuatilia hali inavyoendelea mashariki mwa nchi hiyo hasa maeneo yanayokaliwa na waasi.

Naye mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, Mary Robinson amesema kuwa anaamini majadiliano kati ya kinshasa na Waasi bado yanaweza kufanikiwa na kukomesha mashambulizi dhidi ya Raia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.