Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA

Obama asisitiza bunge litaidhinisha kuishambulia Syria, utalawa wa Assad uko tayari kwa Vita vya Tatu vya Dunia

Rais wa Marekani Barack Obama amesema ana uhakika bunge la Congress litaidhinisha pendekezo lake la kuishambulia Syria kijeshi kutokana na matumizi ya silaha za kemikali.

REUTERS/Jonas Ekstromer
Matangazo ya kibiashara

Obama akiwa ziarani nchini Sweden amesema kuwa hatakubali makosa yaliyofanyika Iraq yajirudie lakini kwa hili la Syria wana ushahidi wa kutosha kuwa silaha za kemikali zilitumika.

Barack Obama amesema kuwa yeye alikua ni miongoni mwa watu waliopinga mashambulizi dhidi ya Iraq na kuongeza kuwa yeye si mtu kuamini taarifa hafifu za kiintelijinsia na asingependa makosa yaliyotokea huko nyuma yajirudie.

Katika hatua nyingine rais huyo wa Marekani amesema ana uhakika kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin atabadili msimamo wake pamoja na watu wengine wa kupinga mashambulizi dhidi ya Syria.

Wakati huohuo Serikali mya Syria imesema kuwa haitishwi na vitisho vya Marekani na washirika wake kutaka kuishambulia kijeshi nchi hiyo na kusema kuwa serikali hiyo imechukua hatua zote zinazostahili kujilinda.

Serikali hiyo ya Syria imeapa kuwa kamwe haitabadili msimamo wake kutokana na vitisho hivyo ambavyo vinalenga kumwadhibu Rais wa Syria Bashar al-Assad hata kama kutatokea vita ya tatu ya dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.