Pata taarifa kuu
SYRIA-UN

Ban Ki Moon ahofia usalama wa raia wa Syria, ataka usambazaji wa silaha ukomeshwe

Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ameeleza wasiwasi juu ya raia 2500 waliokwama mjini Homs wakati huu ambapo vikosi vya utawala vikipambana na Waasi, ili kuudhibiti mji huo.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Ban amerejea wito kuzitaka pande hizo mbili kuepuka madhara dhidi ya Raia na kuruhusu kufika kwa Misaada ya kibinadamu na kutoa fursa kwa Raia waliokwama kuondoka katika maeneo hayo bila hofu yeyote.
 

Ban pia ametoa wito wa kukomeshwa kwa usambazaji wa silaha kwa pande zote nchini Syria na Washirika wake kutazama mbele kutafuta suluhu ya kisiasa kuondokana na machafuko.
 

Majeshi ya Serikali ya Bashar al-Assad yameungana na wapiganaji wa kundi la Hezbollah la Lebanon kupambana na wapiganaji wa upande wa upinzani hali ambayo imechangia kuongezeka kwa mapambano nchini humo.
 

Zaidi ya watu 100,000 wamepoteza maisha tangu mgogoro ulipoanza mwezi March mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.