Pata taarifa kuu
SENEGAL-MAREKANI

Rais wa Marekani Barack Obama na familia yake kuzuru kisiwa cha Goree nchini Senegal

Rais Barack Obama wa Marekani anataraji kuipongeza demokrasia iliokita mizizi nchini Senegal katika duru ya kwanza ya safari yake barani Afrika ambapo anataraji kutembelea jumba lililotumiwa wakati wa biashara ya watumwa iliopo kwenye kisiwa cha Goree, ikiwa ni ziara yenye mfano wa rais wa kwanza mweusi wa Marekani katika kisiswa hicho.

Rais wa Marekani Barack Obama na Macky Sall wa Senegal
Rais wa Marekani Barack Obama na Macky Sall wa Senegal derniereminute.sn
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya Obama, barani Afrika itatamatika Julai 3, baada ya kutembelea nchini Afrika Kusini na Tanzania, hata hivyo, ratiba ya ziara hii inaweza kupanguliwa iwapo kutatokea taarifa ya kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ambaye hali yake imearifiwa kuwa mbaya zaidi katika saa 48 zilizopita.

Rais Obama amewasili jana Jumatano jijini Dakar akiambatana na mkewe Michelle pamoja na wanaye Sasha na Malia atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Macky Sall alhamisi hii na baadae kuendesha mkutano wa pamoja na vyombo vya habari.

Wananchi wa Senegal wamejitokeza kwa wingi kumpokea rais Obama na familia yake ambapo kwenye barabara inayokwenda Ikulu ya rais nyimbo vificho na nderemo ndivyo vina sikika.

Baada ya mkutano na vyombo vya habari raid Obama atakwenda kukutana na jaji wa mahakama kuu nchini humo ambako atahutubia kuhusu utawala bora, ikiwa ni fursa ya kupongeza demokrasia nchini Senegal mtawala wa zamani wa ukoloni wa Ufaransa iliojipatia uhuru wake mwaka 1960 na ambayo haijawahi kutokea mapinduzi na ambako marais wamekuwa wakipishana madarakani kwa amani na utulivu.

Senegal ni moja kati ya nchi zenye utulivu mkuwa katika ukanda wa Afrika Magharibi, eneo linalokumbwa na mizozo ya kisiasa na kijeshi hususan nchini Mali iliotumbukia katika mzozo tangu kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi Machi mwaka 2012, hatuwa ambayo ilipelekea eneo la kaskazini mwa nchi hiyo kuanguka mikononi mwa makundi ya wapiganaji wa kiislam yenye mafungamano na kundi la Alqaeda Waliofurushwa na opersheni ya kijeshi ya majeshi ya Ufaransa na Afrika.

Baadae mchana rais Obama na familia yakd watazuru kisiwa cha Gore na kutembelea katika nyumba iliokuwa ikitumiwa kwa kusafirisha watumwa na mlango maharufu sana wa kuingilia na hakuna kurudi, mlango ambao ulitumiwa kwa waafrika wengi waliosafirishwa kwa nguvu na kupelekwa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.