Pata taarifa kuu
IRAN

Mohammad Reza Aref ajiondoa kama mgombea urais nchini Iran

Rais wa zamani wa Iran Mohammad Khatami anawashawishi raia wa nchi hiyo wanaopenda mabadiliko wamuunge mkono na kumpigia kura Hassan Rowhani, kama rais wa nchi hiyo wakati wa Uchaguzi Mkuu siku ya Ijumaa. 

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kumuunga mkono mgombea huyo imekuja saa chache baada ya kujiondoa kwa Mohammad Reza Aref ambaye alikuwa katika mrengo huo kushawishiwa na kukubali kujiondoa.

Wachambuzi wa siasa za Iran wanasema kuwa hatua ya Rowhani mwenye umri wa miaka 64, kuungwa mkono na marais hao wa zamani kunampa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo dhidi ya wagombea wengine wanaoegemea upande wa kiongozi wa kiroho Ayatollah Ali Khamenei.

Rowhani aliwahi kuhudumu kama mshauri wa rais Khatami kuhusu maswala ya Nyuklia na amesema kuwa ikiwa atashinda urais atafuata nyayo za Khatami na kuhakikisha kuwa anaimarisha uhusiano wa nchi hiyo na Mataifa ya Magharibi.

Wagombea sita watapambana katika uchaguzi huo na atakayeibuka mshindi atachukua nafasi ya rais Mahmoud Ahmadinejad anayemaliza muda wake baada ya kuongoza  nchi hiyo kwa miaka minane.

Miongoni mwa wagombea wengine wanaopewa kipaumbele katika uchaguzi huo ni pamoja na Saeed Jalili, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Mambo ya nje na Meya wa jiji la Tehran Mohammad Baqer Qalibaf.

Iran inasalia chini ya rais Ahmadinejad, imeendelea kuwekewa vikwazo na mataifa ya Magharibi kutokana na mpango wake wa Nyuklia ambao mataifa hayo yanasema ni wa kutengeneza silaha za maangamizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.