Pata taarifa kuu
UINGEREZA-KENYA

Serikali ya Uingereza yatangaza fidia ya £19.9 milioni kuwalipa waathirika wa Vita Vya Mau Mau nchini Kenya

Serikali ya Uingereza imekubali kulipa fidia kwa waathiriwa wa vita vya Mau Mau vilivyofanyika nchini Kenya ambapo taifa hilo lilikuwa linapigana kuhakikisha linapata uhuru kutoka kwa wakoloni. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hague ameliambia Bunge nchini huko kwamba serikali inasikitishwa na kile ambacho kilifanywa wakati wa vita vya Mau Mau na hivyo itatoa fidia yenye thamani ya pauni milioni 19.9.

Wapiganaji wa Kenya walioshiriki kwenye vita vya Mau Mau dhidi ya Serikali ya Uingereza
Wapiganaji wa Kenya walioshiriki kwenye vita vya Mau Mau dhidi ya Serikali ya Uingereza
Matangazo ya kibiashara

Hague amekiri tukio lililofanywa na wanajeshi wa Uingereza kwa kuwanyanyasa na kuwatesa wapiganaji na hata wananchi wa kawaida ambao walikuwa wanadaia uhuru wao katika kipindi cha miaka ya 1950.

Serikali ya Uingereza imetangaza kuwalipa waathirika 5,228 waliopitia madhira mengi kipindi cha vita vya Mau Mau ambapo wanajeshi wa taifa hilo walivamia hadi kambi za raia wa Kenya kipindi cha vita hivyo.

Londona kupitia Waziri Hague imeomba radhi kama ambavyo iliahidi na kisha kutangaza fidia hiyo kutokana na kuguswa na vitendo vya mateso vilivyowakumba wananchi wa Kenya walioshiriki vita vya Mau mau.

Hatua ya Serikali ya London kuomba radhi na hatimaye kulipa fidia inakuja baada ya waathiriwa hao wa vita vya Mau Mau kufungua kesi wakilalamikia utesajwi waliokumbana nao wakati wa vita hivyo.

Waathiriwa hao wa vita vya Mau Mau kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakipambana kuhakikisha wanapata fidia hiyo baada ya kutokea vita vya kudai uhuru vilivyofanyika katika miaka ya 1950.

Keshi hiyo ya kudai fidia ilifunguliwa na Paulo Muoka Nzili, Wambungu Wa Nyingi na Jane Muthoni Mara ambapo walitaka kulipwa fidia naa baada ya mahakama kusikiliza shauri lao wakafanikiwa kushinda kesi hiyo na serikali ikatakiwa kuwalipa fidia.

Askari wa Uingereza wanatuhumiwa kuwatesa raia wa Kenya wakati wa vita hivyo vya Mau Mau lengo likiwa ni kuwatisha ili wasiendelee na harakati zao za kudai uhuru wao kutoka kwa Wakoloni wa Uingereza.

Miongoni mwa vitendo ambavyo vilifanywa na askari hao wa kiingereza ni pamoja na vitendo vya uhalifu wa kijisia ikiwa ni pamoja na kuwabaka wanawake waliokuwa wanaishi kwenye makambi baada ya kukimbia vita hivyo.

Tume ya Kutetea Haki za Binadamu ya Kenya ilionesha watu 90,000 waliuawa kwenye vita hivyo vya Mau Mau kwa kuteswa huku wengine 160,000 waliweka kizuizini bila ya makosa yoyote na kukutana na unyanyasi mkubwa na mateso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.