Pata taarifa kuu
MAREKANI-NIGERIA

Marekani yatangaza zawadi ya dola milioni tano kwa atakayesaidia kukamatwa kwa Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau

Serikali ya Marekani imetangaza zawadi kwa wale ambao watasaidia kutoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa Kiongozi wa Kundi la Wanamgambo wa Boko Haram lenye maskani yake nchini Nigeria Abubakar Shekau.

Kiongozi wa Kundi la Wanamgambo la Boko Haram la nchini Nigeria Abubakar Shekau anayesakwa na Marekani
Kiongozi wa Kundi la Wanamgambo la Boko Haram la nchini Nigeria Abubakar Shekau anayesakwa na Marekani
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetenga jumla ya dola milioni saba kwa ajili ya kupata taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa Shekau hii ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo.

Serikali ya Marekani imetoa orodha ya watu kadhaa ambao inawasaka kwa udi na uvumba wakiwemo Viongozi wa Kundi la AQIM na lile la MUJAO ambao wanafanya shughuli zake katika eneo la Kaskazini na Magharibi mwa Afrika.

Mwanamgambo Mkongwe na Kiongozi wa Kundi la Waasi linalofanya mashambulizi yake katika nchi za Kaskazini na Magharibi mwa Afrika Mokhtar Belmokhtar naye hajanusurika kwenye orodha hiyo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetenga kitita cha dola milioni tano kuhakikisha Belmokhtar anatiwa nguvu huku Kundi lake likitajwa kushiriki kwenye mauaji ya watu zaidi ya ishirini yaliyofanyika nchini Niger.

Kamanda Mwandamizi katika Kundi la AQIM Yahya Abu El Hammam naye ni mrengwa katika msako huo akitajwa kufanya utekajinyara wa watu kadhaa katika eneo la Kaskazini na Magharibi mwa Afrika na ametengewa dola milioni tano.

Dola milioni tatu zimewekwa mahsusi kwa ajili ya yule ambaye atatoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa Kiongozi mwingine wa AQIM Malik Abou Abdelkarim pamoja na Msemaji wa MUJAO Oumar Ould Hamaha.

Serikali ya Marekani kwa sasa inaonekana kuanza kunyoosha makucha yake na kuyagusa makundi ya wanamgambo yanayopatikana Kaskazini na Magharibi mwa Afrika yakiwemo AQIM, MUJAO na Boko Haram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.