Pata taarifa kuu
CAMEROON-CHAD-AFRIKA KUSINI-JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Kiongozi wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize aondoka Cameroon kueleka Afrika Kusini kuomba hifadhi

Rais aliyeondolewa madarakani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize ameelekea nchini Afrika Kusini kuomba hifadhi hatua inayokuja baada ya kuishi uhamishoni nchini Cameroon tangu aondolewe mamlakani mwezi Machi.

Rais aliyeondolewa madarakani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize
Rais aliyeondolewa madarakani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize AFP PHOTO/ SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Bozize ameelekea nchini Afrika Kusini akipitia nchini Kenya huku kukiwa hakuna taarifa rasmi zinazobainisha sababu zilizomsababisha kuondoka nchini Cameroon na iwapo kulikuwa na matatizo baina yake na serikali.

Kiongozi huyo wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati aliyeondolowe madarakani kupitia mapinduzi yaliyofanywa na Muungano wa Seleka ametolewa waranti ya kukamatwa na serikali hiyo mpya.

Serikali ya Rais Michel Djotodia juma lililopita imetoa waranti ya kukamatwa kwa Bozize anayetakiwa kurudi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kukabiliana na mashtaka kadhaa yanayomkabili.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati Alain Tolmo ametangaza makosa yanayomkabili Bozize ikiwa ni pamoja na utekejinyara, mauaji, uhalifu wa kibinadamu na uhalifu wa kiuchumi.

Bozize akiwa na familia yake aliondoka nchini Cameroon kwa kutumia ndege ya kukosi akipitia nchini kenya kabla ya kwenda nchini Afrika Kusini na alipokuwa Younde alikuwa anaishi karibu kabisa na makazi ya rais.

Kiongozi huyo aliondolewa madarakani na kuomba hifadhi nchini Cameroon ambapo aliirushia lawama nzito serikali ya Chad kutokana na kuufadhili Muungano wa Serikali na hatimaye kufanikiwa kumuangusha.

Serikali ya Muungano wa Seleka chini ya Djotodia imeahidi kuitisha uchaguzi katika kipindi cha miezi kumi na nane ili kuhakikisha demokrasia inachukua mkondo wake na hali irejee kama awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.