Pata taarifa kuu
NIGERIA

Maelfu wamzika mkongwe wa fasihi Afrika,Chinua Achebe

Maelfu ya waombolezaji wamehudhuria mazishi ya mwandishi mkongwe barani Afrika na anayefahamika duniani Chinua Achebe kutoka nchini Nigeria.

Nguli wa fasihi ya Afrika na mwandishi bingwa wa Vitabu kutokea nchini Nigeria Chinua Achebe,maisha yake yamefika ukomo akiwa na umri wa miaka 82
Nguli wa fasihi ya Afrika na mwandishi bingwa wa Vitabu kutokea nchini Nigeria Chinua Achebe,maisha yake yamefika ukomo akiwa na umri wa miaka 82 REUTERS/Mike Hutchings/Files
Matangazo ya kibiashara

Mazishi hayo yanafanyika nyumbani kwake katika jimbo la Anambra na kuhudhuriwa na viongozi mashuhuri nchini humo wakiongozwa na rais Goodluck Jonathan.

Achebe alifariki dunia akiwa na miaka 82 mwezi wa Machi mwaka huu baada ya kuugua kwa kipindi kifupi kifo kilichowahuzunisha wasomi wenzake pamoja na wasomaji wa vitabu vyake kote duniani.

Miongoni mwa vitabu maarufu alivyoandika na kusomwa na watu dunia ni pamoja na Things Fall Apart miongoni mwa vingine vingi vilivyozungumzia maswala ya uongozi bora barani Afrika.

Achebe atakumbukwa kama mwanzilishi wa fasihi ya Kiingereza barani Afrika na zaidi ya nakala Milioni 10 ya kitabu chake cha Things Fall apart zimeuzwa duniani.

Hadi kufariki kwake Achebe amekuwa akiishi nchini Marekani kuanzia mwaka 1990.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.