Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA-JORDAN

Marekani yasisitiza lazima Rais Assad aondoke madarakani ndiyo suluhu ya kisiasa itapatikana nchini Syria

Marekani imeendelea kushikilia msimamo wake wa kutaka Rais wa Syria Bashar Al Assad aachie wadhifa wake kama sehemu ya kufikiwa suluhu ya kisiasa ya kumalizwa kwa mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili nchini humo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry ndiye ametangaza msimamo huo wa serikali ya Washington akiwa katika siku yake ya tatu ya kusaka suluhu la umalizwaji wa umwagaji wa damu nchini Syria.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Nasser Judeh
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Nasser Judeh Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kerry ameanika msimamo wa Marekani alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Nasser Judeh na mataifa hayo yote mawili yameonesha utayari kuhakikisha kuna kuwa na serikali ya mpito ili kupata suluhu ya mgogoro wa Syria.

Viongozi hao wawili wamesema wao wapo tayari kusimama kidete kuhakikisha hali ya utulivu inapatikana nshini Syria lakini Rais Assad hapaswi kushirikishwa kwenye serikali ya mpito itakayoundwa kwa kushirikisha serikali na wapinzani.

Tayari Balozi wa Marekani nchini Syria Robert Ford amekutana na Upinzani huko Jijini Istanbul kujadili njia ambazo zinapaswa kufanyika katika kuelekea ushindi dhidi ya Serikali ya Rais Assad.

Kauli ya Kerry inakuja siku mbili baada ya Marekani na Urusi kufikia makubaliano ya kushirikiana katika kumaliza umwagaji wa damu ambao unaendelea nchini Syria na kugharimu uhai wa raia wasio na hatia.

Waziri Kerry pia ametangaza msaada wa dola milioni 100 kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wa Syria waliokimbia katika nchi za jirani ikiwemo Jordan na Uturuki ili waweze kupata mahitaji muhimu ya kibinadamu.

Judeh amesema Jordan kwa sasa imepokea asilimia kumi ya wakimbizi kutoka nchini Syria ambao ni karibu 525,000 na hivyo wanabeba mzigo mzigo ambao utaondoka kama utulivu utarejea Damascus.

Takwimu zinaonesha kuwa wakimbizi elfu mbili wanavuka mpaka kila siku kutoka Syria kukimbilia Jordan wakijiepusha na mapigano yanayoendelea na kudumu kwa kipindi cha miezi 26 sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.