Pata taarifa kuu
DRCONGO-M23-UN

Waasi wa M23 watoa masharti mazito ili warejee katika mazungumzo ya amani DRC

Waasi wa kundi la M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wametoa wito kwa serikali ya DRC kukubali kutia sahihi mkataba wa kuachana mapigano kabla ya kuendelea kwa mazungumzo ya Kampala.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo ya kundi la M23 inakuja huku jitihada za kupeleka kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa ambacho kinakwenda kukabiliana na waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
 

Kundi hilo ambalo limesambaratika katika siku za hivi karibuni na kushuhudia kutoroka kwa wapiganaji wake limeamua kutorejelea mazungumzo wakati huu ambapo Majeshi ya Umoja wa Mataifa yanatarajiwa kupelekwa mashariki mwa Nchi hiyo.

Kundi hilo la waasi limesema kupelekwa kwa jeshi la kimataifa huko mashariki mwa DRC ni kuchochea vita na hatua hiyo haitamaliza matatizo ya nchi hiyo zaidi ya mazungumzo ya amani baina ya waasi na serikali.

Kiongozi wa Kundi hilo Betrand Bisimwa waasi hao wamependekeza kuwepo na mkataba huo wa kukataa mapigano kwa maslahi ya wananchi wa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.