Pata taarifa kuu
Uingereza-Kenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aalikwa Uingereza kushiriki mkutano utakaojadili hali ya Somalia

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye pia mtuhumiwa wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa Kenya wa mwaka 2007 katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC amealikwa na Uingereza kushiriki katika mkutano unaohusu Somalia. 

REUTERS/Marko Djurica
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo inakua safari ya kwanza nje ya Bara la Afrika kwa kiongozi wa Afrika anayekabiliwa na kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC.
 

Mkutano huo utakuwa chini ya uenyeji wa Uingereza na Somalia na utajadili masuala mbalimbali kuhusu mustakabali wa nchi ya Somali ambayo imewahi kukosa serikali imara kwa miaka 20.
 

Nchi za Ulaya na mataifa mengine yenye nguvu yamekuwa na sera za kutokua na mawasiliano ya karibu na watuhumiwa wa ICC mpaka pale tu panapokua na umuhimu wa kufanya hivyo.
 

Uingereza imesema katika mwaliko wake kuwa Kenya ni muhimu sana katika suala la nchi ya Somalia huku ikiwa na wanajeshi 5,000 nchini Somalia na ina wakimbizi wengi wa Somalia kuliko nchi yoyote na ndiyo maana wametoa mwaliko huo kwa Kenyatta.
 

Rais Kenyatta alichaguliwa katika uchaguzi wa Machi 4 mwaka huu na kesi yake katika mahakama ya ICC itaanza kusikilizwa mwezi Julai na yeye mwenyewe amesema kuwa atatoa ushirikiano ingawaje mawakili wake wanataka mahakama hiyo imfutie kesi Kenyatta ombi lililokataliwa na ICC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.